Ibrahim Ajibu mchezaji mwenye bahati mbaya sana kisoka

Ibrahim Ajibu mchezaji mwenye bahati mbaya sana kisoka

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Ibrahim Ajibu amezitumikia klabu za Simba na Yanga kwa muda mrefu lakini amekuwa akiongoza " Kupishana na gari la mshahara"

Alikaa sana Simba akicheza soka la mchangani hamu ya kucheza kimataifa hususani klabu bingwa ikamvaa ikabidi kwa nyodo kubwa na dharau aikache Simba aende Yanga ili acheze Kimataifa hasa Klabu Bingwa lakini Kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwani Simba ndio waliopata nafasi hiyo hivyo Ibracadabra alipishana na gari la mshahara.

Alipoona mafanikio ya Simba na Kufulia kwa Yanga akaona isiwe tabu akaamua kuwachunia viongozi wa Yanga ili arudi Simba akacheze klabu bingwa lakini ng'ombe wa maskini hazai nako Simba kaambulia patupu maana katika mechi mbili walizoambulia hajakaa hata benchi Ibrakadabra kama kawaida yake " kapishana na gari la mshahara.

Maoni yangu.
Ajibu ana kile waswahili tunaita "kimavi"
FB_IMG_1566749531889.jpeg
 
Mbaya zaidi kasajiliwa na Mo ili kuwakomoa Yanga! hivyo kuna walakini kama atapata namba ya kudumu ukijumlisha na aina ya viungo ambao wamejaa pale msimbazi. Namtabiria kusugua benchi hadi pale atakapotolewa kwa mkopo kwenda Namungo fc wakati wa usajili wa dirisha dogo.
 
Mchezaji yeyote anayehama Simba kwenda Yanga au Yanga kwenda Simba huyo hajui aliko. Huwezi kuchezwa ngoma mara mbili mbili upone. Mganga wa Yanga ni mkwe wa mganga wa Simba hivyo dawa yao huichimba shamba moja.
Simba humnunua mchezaji Yanga ili kuififisha Yanga na vivyo hivyo Yanga. Kwa hivyo, mpira wao hauongezeki kwa sababu nia ni kumuona mwingine kapoteza ubingwa msimu huu tu. Huo sio ushindani bali uzuzu
 
Ligi haijakwisha ushasema kapishana na gari la mshahara kwani huko CAF CL tayari ninyi Yanga mmepata chochote?
 
Hiyo bahati mbaya kwa Ajib, ni kwa kuwa Yanga wanefuzu kuingia raundi ya kwanza ya Iigi ya mabingwa Afrika au kuna zawadi Yanga watapata kwa kushinda mechi ya awali?

Vv
 
Hiyo bahati mbaya kwa Ajib, ni kwa kuwa Yanga wanefuzu kuingia raundi ya kwanza ya Iigi ya mabingwa Afrika au kuna zawadi Yanga watapata kwa kushinda mechi ya awali?

Vv
Hivi kiswahili ni lugha ngum kueleweka?
 
Msimu ujao ataondoka tena Simba sijui ataenda wapi maaana huyo ni sawa na Kapeto ni wa hapa hapa,anagundu la kufa mtu hata akioga Ziwa Tanganyika kazi bure labda akaoge mto Msimbazi kwenye maji chumvi
 
Hiyo bahati mbaya kwa Ajib, ni kwa kuwa Yanga wanefuzu kuingia raundi ya kwanza ya Iigi ya mabingwa Afrika au kuna zawadi Yanga watapata kwa kushinda mechi ya awali?

Vv
Naona Yanga wanaumia sana Ajib kuondoka Yanga.
 
Msimu ujao ataondoka tena Simba sijui ataenda wapi maaana huyo ni sawa na Kapeto ni wa hapa hapa,anagundu la kufa mtu hata akioga Ziwa Tanganyika kazi bure labda akaoge mto Msimbazi kwenye maji chumvi
Issue ni pesa, uwe ulaya uwe Tz kama unapesa maisha yanaenda.
 
Naona msimu wa mvua umeanza vyura wanakoroma kila sehemu. eti ajibu ana gundu!!!! cjui ajibu na wewe unaeshinda kwenye key-body siku nzima huku hujui kesho yake nani anagundu.. yaani ndala kuishinda township halafu simba kutolewa ndo tayari ajibu kapishana na bahati.. Kamoni!!! vyura hamko Siriasi kabisa! unataka kutuaminisha kwamab Ajibu mwenye usajili wa mil. 80+ pale msimbazi ana gundu kuliko wale wachezaji wenu wa mil. 30, 25, 15 waliobaki ndala fc??? ...... unataka kumanisha kwamba ndala ndo tayari hivyo mmefanikiwa baada ya kumfunga township?? hapo kilichofanyika ni kwamba mmeongeza nguvu tu ya kuhamasishana jinsi ya kuchangishana kwenye mabakuli,tunawasubiri ligi kuu maana tunajua hamtasogea kokote......
 
Acha mapovu wewe kubali tu kwamba mlizoea kufanya manuva na hiyo ligi kuu nayo itakuwa ngumu kumeza mwaka huu.

Kama mtakuja na dhana iliyowaondoa mapema champions league ubingwa mtausikia kwa jirani.

Sasa hivi mmekuwa kama simba wa kwenye picha ambaye hang'ti ,shut up !
 
Back
Top Bottom