Ibrahim Traore wa Burkina Faso ni mfano hai kuwa ili nchi iendelee inahitaji kiongozi dikteta

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hakika wananchi wa Burkina Faso wanabubujikwa na machozi kwa rais mzalendo waliyenpata🙂.

Ndani ya muda mfupi Ibrahim Traore ameonyesha kwa vitendo nia yake ya kuikonboa nchi yake kutoka kwenye umaskini.

Ameanza ujenzi wa refinery kubwa ya dhahabu yenye uwezo wa kusafisha tani 150 kwa mwaka. Hii ni kuiongezea thamani dhahabu nyingi wanayozalisha.

Amekataa kununuliwa viete na kubaki kutembelea defender ya mwaka 2001.

Amekata asilimia 30 ya mishahara ya mawaziri na kuongezea wafanyakazi wadogo mshahara kwa asilimi 50.

Amenunua matreka 400, pump za umwagiliaji na power tillers kwa ajili ya wananchi vijijini.

Ameanza ujenzi wa bwawa kubwa kwa ajili ya umwagiliaji, maji kwa wtu na kuzalisha umeme.
Anafanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Wagadugu.

Anajenga barabara za lami na SGR kuelekea mpaka Ivory Coast.

Kuwa dikteta haiguarantee kuwa utaleta maendeleo, ndiyo maana Blaise Compaore hakufanya chochote cha maana, lakini maendeleo hayawezi kupatikana kama kiongozi siyo dikteta.
 
Sasa hapo kafanya udikteta gani!
Huyo huwezi kumfananisha na wale wajinga wengine waliokuwa wakifikiria kuua wenzao tu wakidhani wao wangeishi milele.
 
Back
Top Bottom