ICC yambana Bensouda kesi ya Kenyatta

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932

Kiongozi wa mshataka katika mahakama ya kimataifa ICC Fatou Bensouda

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja ili kutoa ushahidi dhidi ya rais wa Kenya, la sivyo aondoe mashtaka dhidi yake.

''Kucheleweshwa kwa kesi hiyo ya Rais Uhuru ni kinyume na maslahi ya haki.'' ilisema.

Rais Kenyatta ni kiongozi wa kwanza wa taifa kufika katika mahakama hiyo tangu ashtakiwe rasmi mwaka 2012 na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu,ambayo ameyakana.

Kiongozi huyo wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kujenga kesi yake dhidi ya kiongozi huyo.

Anasema kwamba mashahidi wamehongwa na kutishiwa maisha huku serikali ya Kenya ikikataa kutoa stakhabadhi muhimu za kesi hiyo.

Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa mwaka 2007 ili kumpatia ushindi aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki na kusema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.



Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyeshtakiwa kwa mauaji katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini humo.

Akikataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuchelewesha kesi hiyo, majaji wa mahakama hiyo walisema kuwa wamempatia wiki moja Bensouda kusema iwapo ataitupilia mbali kesi hiyo ama ushahidi alio nao unaweza kuhimili kesi hiyo kuendelea.

Rais Kenyatta alishinda uchaguzi wa urais mwaka 2013 kupitia usaidizi wa Mwai Kibaki.

Aliitumia kesi hiyo kutafuta kuungwa mkono huku akiikashifu mahakama hiyo ya mjini Hague kwa kuingilia masuala ya Kenya.

Ameshtakiwa na mahakama hiyo kwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.

Takriban watu 1,200 waliuawa katika ghasia hizo huku wengine 600,000 wakiachwa bila makazi.


Source:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/12/141203_icc_uhuru_bensouda
 
Bensouda si ndio mwenye ICC mwenyewe!?
 
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC,Bi Fatou Bensouda amepewa juma moja kuiondoa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya au aeleze kama ana ushahidi wa kuendelea na kesi hiyo. Kuna uwezekano mkubwa kesi hiyo kuondolewa ICC.

Chanzo:BBC Kiswahili
Kapewa amri hiyo na nani?
 
Bensouda alikuwa anategemea ushirikiano kutoka serikali ya Kenya ambayo inaongozwa na huyo huyo Uhuru Kenyatta.

Binafsi sidhani kama Uhuru hana hatia lakini pia sidhani kama kuna ushahidi wa kutosha kumpata na hatia mahakamani kwa sababu ya mambo kama witness tampering n.k.
 
Uhuru kashahonga na kutisha mashahidi wote wa muhimu. Hamna kesi hapa.
 
Pamoja na hayo si kwamba kesi imeishia hapo kwani Ushaidi uliotolewa hapo awali haukutosha sababu ya Raia kuogopa kutoa Ushahidi.
Ni mapema mno kusema kesi hii itaisha lini.
 
Navyojua ICC kuna mwendesha mashitaka na majaji...labda huyo alopewa amri ni mwendesha mashitaka (Chief Prosecutor) mimi namkumbuka Ocampo..alimaliza muda wake...aliye m replace simjui jina...

Mahakama ziko very complicated...watu wanafungwa wasio na hatia...wengine wanaachiwa huru wakiwa na makosa...kuna tofauti kati ya haki na sheria...

Kuna dada mmoja anatokea moja ya nchi za eastern Europe alikuwa anasimulia kuhusu mshitakiwa mmoja sijiu Serbia sijui wapi..naye alikuwa kwenye moja ya mahakama The Hague...unaambiwa jamaa liko mahabusu lakini likipelekwa mahakamani linatumia ishara ambazo zinawaumiza mashaidi kwani ndizo walizokuwa wanatumia wakati wanawachinja...kuna siku shaidi kama hakufa basi alizimia mahakamani baada ya jamaa kuonyesha hiyo ishara...

Na cha kusikitisha hilo lishitakiwa linapelekewa flowers likiwa mahabusu na followers wake...haya mambo si unajua hata Hitler ana wafuasi...sasa victims wanaon ni upuuzi...maana jamaa alikuwa ndani lakini anakula good time...case haiamuliwi...mashaidi wanakufa kwa uzee...

Ndio maana wananchi wanaamuaga kuchukua sheria mkononi...
Ona sasa Egypt...Jeshi si limemuachia huru Mubarak...wa Egypt wamefura...cha kufanya hawana...nadhani wanatamani wangemtia moto tu....
 
Uhuru hasingekua RAIS ushahidi ungepatikana tena mzuri,ila kwa sasa ni ngumu,ila huyu mama FATUMA (MUENDESHA MASHTKA)kashusha eshima ya mahakama.OCAMPO alikua hana mchezo,waafrika hatuwezi kazi,kwanza huyu mama hao wahalifu hawaogopi,ila yule mreno alikua NOMA sana
 
Ocampo alikuwa raia wa Argentina...(na kama nakumbuka before alishakuwa lecturer wa law Harvard)
Nimewai kuona documentary yake moja..si mchezo...kusema movie vile...
Alikuwa anaenda DRC na ndege ndogo ya UN kuwachukua mashaidi..wale watoto waliotekwa na kulazimishwa kuwa rebels...

Hiyo documentary ilikuwa inaonyesha mpaka anavyo interact na wasaidizi wake ofisini...anavyoishi nyumbani kwake...etc...jamaa alikuwa fit

Na mikakati alivyokuwa anafanya ya kutafuta ushaidi...yani nilichojifunza ni kuwa majaji wako pale kum challenge...na yeye ana work hard kutafuta evidence...maana walikuwa wanaonyesha hata alipokuwa ana argue mahakamani...

 



Aliye m-replace Ocampo ndio huyo F. Bensouda
 
nyumba kubwa, Adharusi, Nyani Ngabu,
CJ wa Tz mohamed chande na fatou bensouda walikuwa 2 finalists kwenye process ya kumrithi ocampo.

Wakuu wa AU ndiyo walioamua kum-support mama bensouda kwa hiyo cj mohamed chande akarudi kuendelea na kazi yake Tz.

Now can u imagine mahusiano ya Tz na Ky yangekuwaje with mohamed chande as ICC chief prosecutor huku akimfuatilia Uhuri Kenyatta na Wiliam Ruto?
 
Last edited by a moderator:

ocampo ndiye aliyefanya hii kesi iwe nyonge, hakushugulika kufanya upelelezi huru bali alichukua tu ripoti za NGO na jaji waki. Bensouda aliridhi kesi zisizo kuwa na misingi miema
 

Yes, nimekumbuka huo mchakato...
Afu sijui niliipata wapi kuwa Chief Prosecutor ilibidi atoke Afrika sababu washitakiwa asilimia kubwa wanatokea kwenye ili bara...

Na sijui si waafrika tuna laana au? Maana nilikuwa nasoma soma kuwa japo marais wetu wanalalamika sana kuhusu ICC kuwa haiko fair inashitaki waafrika tu, nasikia in most cases (kama si kesi zote) ni viongozi wetu weeenyeeewe wanaomba msaada wa ICC...


Ila sasa kibao kinaelekea kuwageukia ndio wanaanza kulalama...
Before walikuwa wanashitakiwa rebels tu...wakawa wanaona raha...
Sasa hivi wengi tu wa walio madarakani wana sifa za kuwa ICC candidates..ndio maana upepo umebadilika...

Eti wanataka azimio la kuipinga mahakama...akyanani...
 
Sa kwa nini huyo Bansouda hakujazilizia ushaidi?

Afu kama nakumbuka Kenya ni kama waisema watawahukumu watuhumiwa wenyewe...inawezekana hiyo ilimfanya Ocampo asifanye kazi yake na muda wake ukawa unaisha...

Hii mahakama ni last resort...ni kwa wale wasio na uwezo au sifa ya kutatua matatizo yao nchini mwao sababu ya rushwa kama sisi wafrika...ukiwa kiongozi ni ndoto kuwa convicted...

ocampo ndiye aliyefanya hii kesi iwe nyonge, hakushugulika kufanya upelelezi huru bali alichukua tu ripoti za NGO na jaji waki. Bensouda aliridhi kesi zisizo kuwa na misingi miema
 
Bila washtakiwa wakuu raila na mwai huwezi ukafunga mtu ktk hii kesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…