ICC yatoa msamaha kwa Uhuru Kenyatta

ICC yatoa msamaha kwa Uhuru Kenyatta

Farudume

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
3,946
Reaction score
3,689
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC)yenye Makao yake huko The Hague-Uholanzi imemruhusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria Vikao vyote vya ICC ambavyo ataona vinaingiliana na Majukumu yake kama Rais.Awali ICC ilimkatalia Ombi la kutohudhuria baadhi ya Vikao.Marekani wamekosoa uamuzi huo.
Source;BBC.
 
It would rather sound better if the source said..."Obama amekosoa uamuzi huo"
 
Hiyo bado haiondoi kesi kuendelea na kutiwa hatiani ikiwa atathibitika kuwa na makosa. Bado kitanzi kiko palepale, kwani asipohudhuria mawakili lazima wawepo.
 
Kwa Kiswahili ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (International Criminal Court) na si Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (Court of War Crime)
Mahakama ya Uhalifu wa Kivita(ICC)yenye Makao yake huko The Hague-Uholanzi imemruhusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria Vikao vyote vya ICC ambavyo ataona vinaingiliana na Majukumu yake kama Rais.Awali ICC ilimkatalia Ombi la kutohudhuria baadhi ya Vikao.Marekani wamekosoa uamuzi huo.
Source;BBC.
 
Mhhhh Kesi hii ambayo mkuu wa majaji alikuja Tz kimya kimya kabla ya uchaguzi wa Kenya!!!!! Mhhhhhhhhhh!!! Tusubiri tuone mambo yake!!!!!!
 
Mahakama hii haina ukumu ya kifo (kitanzi)
Hiyo bado haiondoi kesi kuendelea na kutiwa hatiani ikiwa atathibitika kuwa na makosa. Bado kitanzi kiko palepale, kwani asipohudhuria mawakili lazima wawepo.
 
Kwa Kiswahili ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (International Criminal Court) na si Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (Court of War Crime)

Ndio! Mahakama ya kuwahukumu waafrika tu na zile nchi maskini za europe!
Hawa wazungu wanalaana ya Mungu!
 
Tuhuma/kesi bado ipo pale pale mahakama ya ICC ingemfutia mashtaka kabisa why Africam leaders only?
 
Tuhuma/kesi bado ipo pale pale mahakama ya ICC ingemfutia mashtaka Uhuru Kenyatta kabisa, why African leaders only?
 
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) hii leo imetoa masharti kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuhusu kuhudhuria vikao vya kesi dhidi yake katika mahakama hiyo kuanzia Novemba 12 mwaka huu.

Kati ya majaji watatu wanaosikiliza kesi dhidi ya Kenyatta wawili walikubali kumruhusu kutohudhuria kesi dhidi yake huku jaji anayeongoza kesi hiyo Kuniko Ozaki akipinga ombi la Kenyatta.
Hata hivyo Kenyatta ametakiwa kuwepo mahakamani kwa ufunguzi wote wa kesi dhidi yake, hotuba za ufunguzi wa pande zote husika , kusikiliza maoni ya waathiriwa na wasiwasi wao , uamuzi utakapotolewa na vikao vyovyote atakavyotakiwa na majaji kuhudhuria.
Ikiwa itawezekana Kenyatta pia atatakiwa kuhudhuria kikao cha uamuzi wa kesi yake.
Iliamuliwa kuwa ikiwa Rais Kenyatta atakosa kutii masharti hayo , basi huenda majaji nao wakamuondolea faida hizo na kutolewa kwa kibali cha kumkamata.




[h=3]ICC says Kenya president can skip parts of trial [/h]
 
Back
Top Bottom