Idadi kubwa ya waendesha pikipiki ni wabishi, wakorofi na wajeuri

Idadi kubwa ya waendesha pikipiki ni wabishi, wakorofi na wajeuri

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Tunashukuru Wachina kutufikisha vyombo vya moto kama pikipiki. Ila ni moja la janga kubwa katika taifa kuanzia kwenye matumizi yake kufikia kujiingiza kwenye hualifu, uporaji kwa kutumia chombo chenyewe, uporaji wa pikipiki na mauaji yake, ajali za pikipiki na n.k

Tuje kwenye matumizi ya barabara ndio tatizo kubwa. Yani magari yameongoza kubomolewa na pikipiki kuliko kupata ajali zake.

Asilimia watumia pikipiki hujikuta muda wote wao hawana makosa sehemu yoyote hata kama katenda.

Wimbi kubwa la watumia pikipiki za Mchina ni wabishi, wakorofi, wajeuri, sio watu wabusara ndio maana ukienda kituoni unaweza kukuta pikipiki ni nyingi kuliko hata magari yaliyo kuwa na makosa.

Asilimia kubwa waendesha pikipiki hawana leseni.

Serikali kusaidia hili.

1622719075433.png

 
Kwa hiyo sisi madereva wa fekon umeamua kutubagaza bila tashwishwi ? Hatuta kubali wala kuafiki jambo hilo.

Toleo la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka mia kenda na sabini na saba imezingatia na kusema kwa kauli moja na thabiti kuheshimu kila raia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kutokuwabagua raia.

Hivyo sisi madereva wa fekon katika kaumu hii, tunakuasa kwa kauli moja na thabiti, usitubagaze !
 
Tunashukuru Wachina kutufikisha vyombo vya moto kama pikipiki. Ila ni moja la janga kubwa katika taifa kuanzia kwenye matumizi yake kufikia kujiingiza
Na waendesha bajaji pia, ni wakorofi sana sana na hawajui sheria za barabarani. dawa yao kuweka ngao mbele na unawafuata kwa spidi ya kutosha manake utakuta amekuja kwenye saiti yako amekulenga kabisa kama anajua gari yako ni laini. pia wanaringa kwamba ukimgonga mmoja wanakuja mia na hapo utakiona kilichompiga mkoloni kama sio kibanga.
 
Siyo wabishi, wengi hawajui kitu kinaitwa safety, usipojua safety ni Nini utaonekana hovyo
 
Unachosema Ni Kweli
Ila Hao Ni Wapiga Kura Wa Ccm
 
Bodaboda Mkuu watu weifanya ya kukwepea majukumu. Kijana wake akipiga 'O', straight kwenye duka la bodaboda, hata kama ni kwa mkopo. Halafu kwa kijana wake: "Haya nakukabidhi hii hapa, hangaika, sitaki shilingi yako, ndiyo mtaji wako. Chapa mwendo"
 
Nilijionea vijana wa bodaboda kule mbeya wakimchoma moto jamaa mmoja wakimtuhumu kua yule jamaa alimua mwenzao na kumpora pikpk
 
Wana inferiority complexity ya dhidi ya wenye magari. Yaani unakuta boda boda anakamata lane nzima anakomaa nayo jamani hatembelei pale kwenye shoulder hatembei anajiona yeye ni sawa na gari. So anataka apewe heshima
 
Bodaboda hawajui brake iko wapi wanachojua wao ni honi tu. Wasenge sana hawa jamaa.
 
Issue ni malezi toka utotoni, tabia haifundishwi ukubwani,ni ngumu sana kumbadili mtu ambaye tayari kajaza midevu.
 
Tuseme ukweli tu, bodaboda wengi ni vijana wa hovyo sana. Mie Nina jamaa mtu mzima nimemkabidhi pikipiki jamaa anaendesha kwa nidhamu mpaka natamani ningekuwa na wengine wawili niwape pikipiki Ila Hawa wanyoa viduku siwezi kuchezea hela yangu heri nikalewee tu.

Unaweza kuishiwa kugombana na kijana asiye na mbele Wala nyuma
 
Back
Top Bottom