Idadi wafanyakazi wachina barani Afrika yapungua, wenyeji waliopata mafunzo wachukua nafasi zaidi

Idadi wafanyakazi wachina barani Afrika yapungua, wenyeji waliopata mafunzo wachukua nafasi zaidi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111166413093.jpg

Katika siku za hivi karibuni takwimu kutoka Idara ya utafiti wa mambo ya China na Afrika (CARI) katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani, zilionesha kuwa idadi ya wafanyakazi wachina barani Afrika imepungua kwa zaidi ya nusu ikilinganishwa na mwaka 2015 ilipofika kilele, tangu takwimu kuhusu wafanyakazi hao zianze kukusanywa.

Mwanzoni kwenye miaka ya 2000 wakati wakandarasi wa China walipoanza kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi barani Afrika, makampuni ya China yalikwenda na wafanyakazi wengi kutoka China hali iliyozusha maswali. Lakini ukweli ni kwamba makampuni mengi ya China yaliyokwenda kutekeleza kandarasi barani Afrika yalisahau kujiandaa kwenye vipengele vya lugha, utamaduni na hata sheria za nchi wanakokwenda, ndio maana ilikuwa ni rahisi kwa makampuni hayo kuajiri wafanyakazi wachina na sio wenyeji, hasa kwenye kandarasi ambazo zilitakiwa kukamilishwa haraka. Kutokana na hali hiyo tunaweza kuona kuwa kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2015 idadi ya wafanyakazi wa China iliendelea kuongezeka na kufikia kilele.

Baada ya hapo, kutokana na makampuni ya China kutambua changamoto za lugha, utamaduni na desturi za wenyewe, na wenyeji kutambua desturi za wachina kwenye kufanya kazi, polepole maelewano yakaanza kuimarika, na makampuni ya China yakaanza kuwa na uwiano kati ya wafanyakazi wachina na wenyeji. Na hatimaye sasa kwenye miradi mingi inayotekelezwa na makampuni ya China barani Afrika, iwe ni ile ya makampuni ya serikali ya China au hata ya makampuni binafsi, idadi ya wafanyakazi wenyeji ni kubwa kuliko ile ya wafanyakazi wachina.

Kipengele muhimu ambacho kinastahili kutajwa ni mkakati wa muda mrefu wa China katika kuisaidia Afrika. Tukumbuke kuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, China imekuwa ikihimiza mpango wa kusafirisha teknolojia kwenda Afrika, na hili linafanyika kwa kualika watu wa Afrika kuja kupata mafunzo nchini China, na kupelekea wataalam wa China kufanya kazi na kuwapatia ujuzi wenyeji. Kupitia mchakato huu wafanyakazi wenyeji sio tu wameweza kupata ujuzi ambao hapo awali hawakuwa nao, lakini pia wameweza kujifunza utamaduni wa kazi wa wachina, na wameweza kushirikiana kirahisi zaidi na wachina ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.

Hata hivyo baadhi ya watafiti wa nchi za magharibi wamekuwa wakizusha hoja zisizo na msingi. Kama ilivyokuwa mwanzo, walitumia uwepo wa wafanyakazi wengi wachina kukosoa ushirikiano kwenye uendeshaji wa miradi kati ya China na Afrika, na sasa wanatumia kupungua kwa idadi ya wafanyakazi wa China kukosoa ushirikiano. Lakini ukweli unaonesha kuwa mkakati wa muda mrefu wa mafunzo kwa wenyeji na kuendeleza nguvu kazi ya wenyeji, unaonekana kuwa umepata mafanikio makubwa.
 
Back
Top Bottom