" Idadi ya goli tutakazofunga itategemea na shauku aliyonayo mpinzani wetu dhidi yetu.''

" Idadi ya goli tutakazofunga itategemea na shauku aliyonayo mpinzani wetu dhidi yetu.''

Gochavez

Senior Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
171
Reaction score
155
Hii kauli imebeba maana kubwa sana leo unajua kwanini unapocheza na Yanga kisha ukapata shauku sana ya kufunguka na kuwashambulia ndipo hapo unaingia kwenye mtego wao.

Ukiwashambulia Yanga kisha ukaacha sana magepu kwenye zone yako ombea Yanga wasiupate huo mpira ni wazuri sana kwenye kufanya transitions ya kukushambulia ambapo mara nyingi wanapenda kupiga pasi zinazovunja mistari yako zaidi ya miwili au mitatu kutegemeana na magepu mliyoyaacha.

Unapowashambulia sana Yanga hakikisha huachi magepu sana kwenye zone yako je inawezekana kuacha magepu makubwa wakati unaona mpinzani wako amerudi nyuma na unaona una nafasi ya kumfunga hapo ndipo mtihani ulipo na ndipo mtego ulipo.

Magoli mengi ambayo Simba amefungwa na Yanga ya Gamondi mara nyingi amekuwa akiwawekea huu mtego na wananasa.

Fadru awe makini sana leo kwenye mbinu yake. Ukitaka kuwafunga Yanga wape wao mpira kisha wavizie waje wakushambulie. Je Fadru atakubali Yanga awe na umiliki mkubwa sioni hilo likitokea.
 
Ukitazama kikosi cha Yanga kuanzia Kipa mpaka mshambuliaji, sio rahisi kuona mapungufu.

Upande wa Simba mapungufu yanaonekana kila eneo na hii ni kutokana na kutofanya usajili wa kiwango cha juu. Siioni Simba yenye matokeo chanya dhidi ya Yanga leo.

Technically, Morale Yanga iko juu zaidi kuliko Simba. Hii mechi Simba asipokuwa makini atafungwa goli zisizopungua 3.
 
Back
Top Bottom