Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Idadi ya maiti Shakahola yafikia 403
Idadi ya maiti zilizofukuliwa katika msitu wa Shakahola imefikia 403 baada ya miili 12 kufukuliwa tena. Hayo yamethibitishwa na Kamishna wa ukanda wa pwani Rhoda Onyancha ambaye amesema shughuli ya kusaka miili inaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai DCI.
Mshukiwa Mkuu Mchungaji Mackenzie bado anashikiliwa na polisi huku uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
Aidha watu zaidi ya 9 wamekamatwa kuhusiana na mkasa huo unaotajwa kuwa hatari zaidi katika historia ya Kenya.
########
Updates...
KENYA: MIILI YA WATU 16 YAFUKULIWA SHAKAHOLA, IDADI YAFIKIA 419
Ongezeko la miili hiyo limepatikana Julai 18, 2023 wakati kwa jumla watu 95 wameokolewa na Vyombo vya Usalama tangu kuanza kwa mchakato huo, ikiaminika Mamia ya Wafuasi wa Kanisa la Kimataifa la Habari Njema, walifariki kwa njaa, kupigwa vibaya au kukabwa katika Msitu wa Shakahola.
Hakuna mtu wa ziada ambaye amekamatwa kwa siku za hivi karibuni na uchunguzi wa kubaini miili eneo la tukio unatarajiwa kuendelea Julai 20, 2023.
Chanzo cha matukio hayo inatajwa ni #PaulMackenzie ambaye anashikiliwa akidaiwa kuhubiri kuwa mwisho wa Dunia unakaribia, hivyo kuwashawishi wafuasi wake kufa kwa njaa ili waweze kumwona Yesu, uchunguzi dhidi yake unaendelea.
#####
16 More Bodies Recovered From Shakahola Forest As Death Toll Rises To 419
Sixteen more bodies were on Tuesday exhumed at the mass graves site in Shakahola Forest, Kilifi County.
The official death toll is currently at 419 with 95 persons having been rescued by law enforcement authorities who are currently in the fourth phase of the exhumation process.
According to Coast Regional Commander Rhoda Onyancha, no new arrests have been made in connection to the recovered bodies; as such total arrests remain at 37 while 258 DNA samples have been collected so far.
The exhumations will continue on Thursday.
Self-proclaimed pastor Paul Mackenzie of the Good News International Church is currently being held by police in connection to the recovered bodies believed to be his followers who starved themselves to death 'in order to meet Jesus'.
Source: Citizen Digital