joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Wizara ya Afya ya Kenya imesema kwamba idadi ya watu wenye virusi nchini humo inategemea kuongezeka kwa kasi sana na kufikia watu 10,000 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa, hii itakuwa ni idadi kubwa kuliko nchi yoyote hapa Africa.
Tamko hili toka kwa hawa majirani linaonyesha wazi ni kwa kiasi gani serikali ya Kenya ilivyodhaifu katika kukabiliana na hili tatizo. Wakati ambapo nchi ndogo ya Rwanda imetangaza kuzuia raia wa nchi nzima kutotoka nje " Total lockdown" idadi ilipofika 40, Kenya bado hawaonyeshi dalili yoyote ya kufanya hivyo na hakuna mipango yoyote madhubuti ya kupunguza kasi hiyo zaidi ya kupima na kutangaza walioathirika.
Hii nchi inasababisha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kuwa magumu sana katika ukanda huu kutokana na uzembe wa viongozi wa Kenya kama kawaida yao miaka yote.
Sent using Jamii Forums mobile app