beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Maelfu ya watu wamejiunga na wimbi jipya la maandamano dhidi ya sheria mpya ya uraia nchini India huku idadi ya waliokufa katika vurugu hizo za karibu wiki mbili ikifikia watu 23.
Idadi ya vifo imepanda siku moja baada ya kuzuka maandmanao ya vurugu kwenye jimbo la Uttar Pradesh ambako watu 15 akiwemo mtoto wa miaka 8 waliuwawa.
Hasira inaongezeka juu ya sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mnamo Disemba 11, inayotoa nafasi ya kupatiwa uraia wahamiaji wasio waislamu kutoka jamii za wachache kwenye mataifa matatu yaliyo jirani na India.
Wakosoaji wake wanasema sheria hiyo inawabagua waislamu na ni sehemu ya mpango wa chama cha kihindu cha waziri mkuu Narendra Modi, madai ambayo mwenyewe amekanusha.
Mamlaka za India zimetakangza sheria za dharura, kzima mtandao wa intaneti pamoja na kufunga maduka kote nchini humo ili kujaribu kudhibiti vurugu zinazoendelea.