Idadi ya walionyongwa tokea uhuru Tanzania ni 232

Idadi ya walionyongwa tokea uhuru Tanzania ni 232

Mlendamboga

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
667
Reaction score
338
Takwimu kutoka kamisheni ya haki za binadamu Tanzania inaonesha kuwa kati ya watu 2,478 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa kufikia mwaka 2010, ni watu 232 waliotekelezewa hukumu hiyo ambayo ni sawa na 9.39%.

Sehemu kubwa ya watu hao walinyongwa awamu ya kwanza ya rais Nyerere na hii ilitokana na mazingira ya wakati huo kiutawala ambayo wakati mwingine yalilazimu maamuzi hayo ili mambo yenye maslahi mapana ya nchi yaende!
 
Kimsingi ni mjadala mzuri, kulingana na zoezi la ukusanyaji maoni lililofanywa na kamisheni ya haki za binadamu nchini wengi wanashauri ifutwe lakini wakitoa mazingira!!! hii inamaanisha kuwa waliowahi tokewa na matukio ya kuuliwa ndugu zao wanapenda adhabu hii kwasababu ya jazba, lakini je ni kweli kwa adhabu hiyo kuna suala la mtuhumiwa/mhukumiwa kujifunza baada ya kutumikia adhabu? rejea lengo la adhabu ni kumfunza aliyekosa! je kwa kumuua, atakuwa amejifunza?
 
nadhani ni pamoja nazo hasa kwenye issue ya uhaini!!
 
Naona hyo adhabu ifutwe..lengo la adhabu ni kumfundisha mhalifu..ukimwua hakuna alilojifunza na wote n km kundi moja
 
Inasemekana kwamba tangu uhuru aliyenyongwa ni Mwamwindi pekee, (aliye mpiga risasi dk.klerruu),wengine mwl.pamoja na marais waliomfuata kamwe hawakutia saini,matokeo yake hupelekwa ktk gereza maalum na hujifia kifo cha kawaida,maradhi au uzee.
 
Hapana hizi ni takwimu zilizotolewa na kamishna wa Tume ya haki za binadamu Jaji Francis George Mlawa, that means ni chanzo sahihi cha Taarifa
 
Msimsingizie Nyerere!!! Alisaini hukumu ya muuaji wa Dr. Kleruuu!!! Wegine waliohukumiwa kufa hakusaini na wengine walizeeka na kufa wenyewe!!! Hadi leo Tanzania ni nchi ambayo imekuwa ikiwahifadhi sana wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na mpaka kuna kipindi walikuwa wanalalamika!!!!! Nashangaa eti mtu anauliza eti alihukumiwa kunyongwa na amekaa miaka 20 hajanyongwa!!! Mimi ningekaa kimya tu hadi nife tu mwenyewe!!! Hata mfungwa ana haki ya kuishi!!! Cha msingi kwa Tanzania ukihukumiwa kunyongwa ni kama vile tu umefungwa kifungo cha maisha!!! Ni kwa kuwa pia adhabu vya vifo hazitokei mara nyingi sana!!! Hukumu yake must be proven beyond reasonable doubt!!! Mahakimu hao hapa wanadata maana kumwaga damu ya mtu si mchezo!!! Nao wanageuka binadamu wanajaribu kutafuta vifungu vya kupooza adhabu ya kifo pale inapowezekana!!
 
Inasemekana kwamba tangu uhuru aliyenyongwa ni Mwamwindi pekee, (aliye mpiga risasi dk.klerruu),wengine mwl.pamoja na marais waliomfuata kamwe hawakutia saini,matokeo yake hupelekwa ktk gereza maalum na hujifia kifo cha kawaida,maradhi au uzee.

Nayajua magereza yote ya Tanzania bara, hilo gereza maalum ndio gereza gani?
 
Lakini pia ukirejea yule mtanzania aliyeomba kazi ya kunyonga Botswana kama siyo Namibia, katika cv yake aliyoiweka hadharani miaka Fulani na ikaandikwa sana kwenye magazeti ya bongo alionyesha kunyonga watu 40 mikononi mwake akiwa anafanya kazi ya kunyonga kwenye gereza la pale mjini Dodoma!!! Hii inathibitisha kuwa ni zaidi ya 1 ya Mwamwindi!!!
 
Kwa hali tuliyo nayo kiutawala sasa hv wandelee kunyonga tu aiisee!
 
EEEEEEEE, KIBOKO10 kulikoni hebu funguka, hali ya sasa ikoje???
 
nadhani ni pamoja nazo hasa kwenye issue ya uhaini!!

Kesi za "uhaini" tanganyika zilikuwa 3.
1: tarehe 20 jan 1964 jeshi tanganyika rifles lilitaka kuasi.
2: Mwaka 1969???? Akina bibititi na mnanka na wenzao(kambona rip)
3:1984 desemba akina Hatty gandh mcghee uncle tom.hans pope. eugene maganga. et al
Hakuna mhaini aliyehukumiwa kunyongwa.
 
Adhabu ya kunyongwa ibaki milele ila iwe strict kwa wanaoua kikatili....huwezi kueleweka kua mtu anayeua kwa kumchinja binadam bila kughadhibishwa naye ataonewa akinyongwa pia....
 
hivi kikwete hajawahi kusign mtu kunyongwa?
 
Back
Top Bottom