Kuzaa inategemea uwezo wa kuzaa na uwezo wa kutunza. Unaweza kusema unataka 2, kumbe hata ukishapata huyo 1 ndiyo huwezi tena, kiafya (nimeshaona mfano). Na pia unaweza kutaka wengi na ukawapata wakakushinda kutunza. Lakini wapo pia waliopata watoto wengi (8, 10 au zaidi) na wamewatunza wote vizuri, inategemea na walivyojizatiti kiuchumi na kijamii, na uimara wa uhusiano wao kama familia.
Kama ni suala la utafiti, ni vigumu kupata idadi ya wastani ya watoto ambao unaweza kupendekeza wanandoa wazae, maana hayo masuala ya social and economic stability yanatofautiana sana baina ya watu.
Mimi nitazaa wangapi? Nitaangalia hali itakavyokuwa wakati huo ninapozaa, na kama yapo matumaini ya improvement. Nilishaona mtu fulani alizaa watoto 2 tu kwa sababu eti hali yake ya uchumi ilikuwa mbaya. Lakini wale 2 walipomaliza sekondari, biashara zake zikamkubali akapata pesa nyingi sana. Akaanza kubwabwaja kuwa angejua angezaa wengi zaidi. Sasa ya nini kujilaumu baadae?
Tunaishi kwa matumaini kuwa hali itakuwa bora huko baadae kutokana na bidii tunazofanya. Hivi kama mimi sasa hivi naishi chumba cha kupanga, niogope kuzaa ati kisa sina nyumba? Sasa nikifika miaka 50 nikapata nyumba yangu mwenyewe, nikizaa muda huo nitatunzaje hao watoto.
Namalizia hivi: Kama unaweza mahitaji ya kawaida ya mtoto kwa wakati huu, zaa. Kama una wawili na hushindwi kumlisha wa 3, na huna shida za kiafya, zaa. Endelea hivyo, hata wakifika 5, 6, 7 nk, idadi ya mwisho ya watoto itajileta yenyewe kulingana na hali ya wakati huo unapofikiria kuzaa mwingine.