idadi ya watoto vs maisha bora



Nakukubali,nimeona hili kwa sana mitaani,wasomi wana watoto wachache tatizo wanaogopa maisha eti maisha ni magumu, sasa suala la kuogopa maisha ni kitu ambacho kwa mtazamo wangu naona kama ni kinyume na mapenzi ya Mungu (kama sikosei) wakati Mungu mwenyewe ndo hutoa neema ya kuzaa watoto kadhaa katika familia.

Wewe unaweza ukasema nitazaa watoto labda wawili(2), wakati Mungu pengine amepanga mzae watoto labda wanne(4) au watano(5). Kwa mtazamo ki-Mungu ni kwamba unao uwezo wa kutunza watoto wengi tu.

Msiogope maisha jamani.Mwombeni Mungu atawaongozeni na kuwajulisheni mzae wangapi na malezi ya watoto pia atawapa maarifa ya kuwatunza.

Kwa Mungu kila kitu kinawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…