Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya Duniani imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022

Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya Duniani imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC .

Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya ulimwenguni imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.

Akizindua ripoti hiyo jijini Vienna Austria Mkurugenzi Mkuu wa UNODC Ghada Waly ameeleza kuwa uzalishaji wa dawa za kulevya na matumizi yake unazidisha ukosefu wa utulivu na usawa wakati huo huo ukisababisha madhara makubwa kwa afya, usalama na ustawi wa watu.

“Tunahitaji kutoa matibabu yaliyofanyiwa uchunguzi na kuwa na Ushahidi wa kuweza kusaidia wale walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya huku tukilenga soko haramu la dawa za kulevya na kuwekeza zaidi katika kuzuia matumizi ya dawa hizo.” Amesema Bi. Waly.

Matumizi ya bangi yamesalia kutumika zaidi duniani kote ambapo kuna watumiaji watumiaji milioni 228, ikifuatiwa na dawa nyingine ambazo ni opioids yenye watumiaji milioni 60, amphetamines yenye watumiaji milioni 30, cocaine watumiaji milioni 23, na ecstasy ikiwa na watumiaji milioni 20.

Ripoti hiyo imetangaza kuwekwa rekodi mpya ya juu ya uzalishaji wa cocaine tani 2,757 mwaka2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 zaidi tangu mwaka 2021.

Matumizi wa bangi umeongezeka kwa kiasi cha mara nne katika sehemu mbalimbali duniani katika kipindi cha miaka 24 iliyopita.

Watumiaji wanakosa matibabu
Ingawa wastani wa watu milioni 64 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya, ni mtu mmoja tu kati ya 11 anayetibiwa.

Wanawake wanapata huduma ndogo zaidi za matibabu ikilinganishwa na wanaume. Ni mwanamke mmoja tu kati ya 18 mwenye matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya ndio anapata matibabu ikilinganishwa na mwanaume mmoja kati ya saba.

Kwa mujibu wa utafiti huo wa mwaka 2022, inakadiriwa kuwa watu milioni 7 walikamatwa au kupewa onyo au tahadhari na polisi kwa makosa ya matumizi ya dawa za kulevya, na karibu theluthi mbili ya jumla hiyo kutokana na matumizi ya dawa za kulevya au kupatikana kwa matumizi.

Aidha, watu milioni 2.7 walifunguliwa mashitaka kwa makosa ya dawa za kulevya na zaidi ya milioni 1.6 walitiwa hatiani duniani kote mwaka wa 2022, ingawa kuna tofauti kubwa katika kanda mbalimbali za ulimwengu kuhusu mwitikio wa haki ya jinai kwa makosa ya dawa za kulevya.

Ni haki yao kupata matibabu
Ripoti hiyo imeeleza jinsi haki ya afya ni haki ya binadamu inayotambulika kimataifa ambayo ni ya binadamu wote, bila kujali hali ya mtu kutumia dawa au kama mtu kuwekwa kizuizini, au amefungwa.

UNODC inasema haki hiyo inatumika sawa kwa watu wanaotumia dawa za kulevya, watoto na familia zao, na watu wengine katika jamii zao hivyo nchi zinapaswa kuheshimu na kutekeleza haki hiyo kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

Athari kwa jamii na mazingira
Katika athari nyingine kwa jamii UNOCD imesema wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameingilia katika nyanja nyingine za kiuchumi ambazo ni haramu ikiwemo usafrishaji wa wanyamapori, ulaghai wa kifedha na uchimbaji haramu wa rasilimali.

Jamii za wakimbizi, wahamiaji na watu masikini wamejikuta matatizoni kwani wamekuwa wakilazimishwa kugeukia kilimo cha Opium au uchimbaji wa rasilimali haramu ili kuweza kuishi, jamii hizo pia zimejikuta zikitumbukia katika mtego wa madeni na vikundi vya uhalifu, au wao wenyewe kutumia dawa za kulevya.

Shughuli hizi haramu pia zinachangia uharibifu wa mazingira kupitia ukataji miti, utupaji wa taka zenye sumu, na uchafuzi wa kemikali.

Soma ripoti hiyo yote hapa World Drug Report 2024 homepage
 
Hapo kwenye bangi Nakubali, hasa hivi vibinti vya "efu mbili" vinakula "mpepe" Kama videge moshi, tena usipovuta wanakuona mshamba uliepitwa na wakati.
 
Zamani msela ukionekana unavuta sigara bwege ulikuwa unaonekana muhuni na kuogopwa mtaani, siku hizi ndio unapendwa nakuonekana mjanja.
 
Unga sio issue tena kwenye maeneo ya starehe madogo wanapyenga kama hawana akili nzuri, tena kwa kufwata mkumbo.

Weekend moja kwenye house party mahali fulani tulikuwa na mutual friends wapopo (naija), basi mwenyeji wao (mbongo) akawaletea pisi za "efu mbili" zimenyooka hatari, basi kama unavyojua wapopo linapokuja swala la kuspend, hapo mezani Ni mwendo wa Hennessy, Jack Daniels, Moet, baada ya muda watu wakaanza "kupyenga" , saa ngapi vile vitoto vianze kuiga! Well kuja kuamka asubuhi wengine wamelala vyooni hawajitambui, wengine wakaishiwa kufi****. Hizi starehe za kukurupukia sio nzuri wadogo zetu.
 
Unga sio issue tena kwenye maeneo ya starehe madogo wanapyenga kama hawana akili nzuri, tena kwa kufwata mkumbo.

Weekend moja kwenye house party mahali fulani tulikuwa na mutual friends wapopo (naija), basi mwenyeji wao akawaletea pisi za "efu mbili" zimenyooka hatari, basi kama unavyojua wapopo linapokuja swala la kuspend, hapo mezani Ni mwendo wa Hennessy, Jack Daniels, Moet, baada ya muda watu wakaanza "kupyenga" , saa ngapi vile vitoto vianze kuiga! Pombe kali+ Mpepe+ poda vikazima. Well kuja kuamka asubuhi wengine wamejikuta wapo vyooni hawajitambui, wengine wakaishiwa kufi****. Hizi starehe za kukurupukia sio nzuri wadogo zetu.
 
Back
Top Bottom