Idara ya Katiba kuwasaka wasiojisajili

Idara ya Katiba kuwasaka wasiojisajili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
_DSC0058.JPG

NA HAJI NASSOR, PEMBA

MKURUGENZI wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, amesema msako mkali unakuja kuwabaini watu na taasisi, zinazofanyakazi za kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria, pasi na kujisajili kama sheria inavyotaka.

Alisema, Sheria ya namba 13 ya mwaka 2018 ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, inamtaka mtu yeyote au taasisi inayotaka kujishughulisha na kazi hiyo, kwanza kujisajili, ili kuwa halali kufanya kazi hiyo.

Alieleza kuwa, Idara imebaini wapo watu na hata taasisi zinaendelea kutoa ushauri, msaada na elimu ya kisheria, bila ya kujisajili, jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria hiyo.

Mkurugenzi Hanifa, aliyasema hayo Septamba 16, 2023 ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makoyo Wawi Chake chake Pemba, wakati akijibu hoja za baadhi wa wahusika wa msaada wa kisheria, kwenye mkutano wa nusu mwaka, ambao umeandaliwa na Idara hiyo, kwa kushirikiana na UNDP.

Alieleza kuwa, msako utanzia katika wilaya za Wete, Micheweni, Chake chake na kumaliza wilaya ya Mkoani kwa Pemba, kisha kuhamia kisiwani Unguja.

Alieleza kuwa msako huo, hauna nia mbaya bali ni kuitekeleza kwa vitendo sheria ya Msaada wa kisheria ya Zanzibar, ambayo imelekeza mambo kadhaa, likiwemo la kujisaliji.

Aidha Mkurugenzi Hanifa, alisema jingine ambalo wameligundua ni kuwepo kwa Mawakili nao kijisajili kama wasaidizi wa sheria, jambo ambalo ni kosa kubwa zaidi.

‘’Ni kweli kati ya wasaidizi wasaidizi wa sheria 250 kwa Unguja na Pemba ambao hadi sasa walioshajisajili hawafiki hata nusu yake, na kwa upande wa wa Mawakili nao wapo waliojisajili kama wadaidizi wa sheria, wakati tayari tunakuja,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Katiba na Sheria Zanzibar kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, alilipongeza shirika la UNDP kwa kuendelea kuwaunga mkono, katika shughuli zao mbali mbali.

‘’Hata mkutano huu wa nusu mwaka kwa wahusika wa msaada wa kisheria Zanzibar, wametusaidia kwa asilimia kubwa, na ndio maana hata washiriki kutoka kisiwa cha Unguja leo tunao,’’alieleza.
_DSC0147.JPG
Aidha aliwakumbusha wasaidizi wa sheria, kuendelea kuifikia jamii, kuwaelimisha athari za udhalilishaji, migogoro ya ardhi, utelekezaji na rushwa, kwani ndio msingi mkuu wa kazi zao.

Hata hivyo amewakumbusha wasaidizi hao wa sheria kuwa, bado nia ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi wa ununuzi wa bajaji kwa taasisi 11 za wasaidizi wa sheria Zanzibar, bado ipo pale pale.

Akifungua mkutano huo, Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Halima Khamis Ali, alisema kazi inayofanywa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, ni kubwa kwa jamii na taifa.

Alieleza kuwa, Mkurugenzi wake amekuwa akizaa mbinu na juhudi binafsi, kuhakikisha wasaidizi wa sheria na taasisi zao zinafikia malengo yao waliojipangia.

Aidha aliwasisitiza wasaidizi hao wa sheria, kuendelea kufanyakazi zao kwa ushirikiano, na taasisi nyingine, ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, alisema wakati umefika sasa kwa taasisi nyingine, kuongeza ushirikiano na wasaidizi wa sheria wanapokuwa na shughuli zao.

‘’Kwa mfano mabaraza ya miji, halmshauri na Manispaa, wanakuwa na shughuli kadhaa, kama za kuandaa sheria ndogo ndogo, msisite kutushirikisha,’’alifafanua.

Afisa sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar Ali Haji Hassan, alisema kazi zinazofanywa na wasaidi wa sheria zitakuwa na uhai, ikiwa wenyewe watajiendeleza kielimu.

Baadhi ya washirika wa mkutano huo, akiwemo Fatma Khamis kutoka ZAPAO, alishauri kuwa, kunapokuwa na mikutano yao mikubwa ni vyema kuwepo na vipeperushi maalum.

Mkutano wa nusu mwaka ulijadili mambo kadhaa, ikiwemo tathimini na mwelekeo wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mwaka 2023, maandalizi ya jukwaa la tatu la mwaka la maaada wa kisheria pamoja usajili wa watoa msaada wa kisheria.

Chanzo: pembatoday
 
Back
Top Bottom