DOKEZO Idara ya kazi na ajira naomba ifuatilie kampuni ya uchimbaji visima, supreme water well drilling limited inawanyima wafanyakazi wake haki za msingi

DOKEZO Idara ya kazi na ajira naomba ifuatilie kampuni ya uchimbaji visima, supreme water well drilling limited inawanyima wafanyakazi wake haki za msingi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya uchimbaji visima, SUPREME WATER WELL DRILLING LIMITED iliyo na makao makuu yake jijini Mwanza, ni muda mrefu umepita tangu nianze kazi katika kampuni hii.

Sijawahi kupewa kadi ya NSSF wala mkataba wa muajiri wangu licha ya kukatwa hela ya NSSF na hata pale wafanyakazi wengine wanapoacha kazi basi hawapewi zile stahiki zao.

Naomba idara inayohusika na ajira na kazi itusaidie kwa hili kwa kuwa tumekuwa tunashindwa kusema popote kutokana na boss wetu kututishia kuwa ikitokea mtu akasema sehemu yeyote basi mtu huyo atafukuzwa kazi.

Hivyo naomba mtusaidie kwa hili.
 
Back
Top Bottom