Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Taarifa iwafikie Idala ya Maji safi na maji taka mkoa wa Mbeya.
Hivi huwa mnautaratibu wa kukagua chemba za maji taka hapa jijini maana mji mzima umekuwa ukinuka harufu ya maji taka.
Mwanzo ilikuwa chemba ya pale Sabasaba karibu na ofisi za CCM, ilikuwa ikivujisha maji taka kwa muda mrefu sana mpaka ile njia ikawa haipitiki tena.
Sasa hali kama hiyo ya chemba kuziba na maji taka kuzagaa mtaani imejitokeza eneo la Sangu Secondari njia ya kwenda Forest ya zamani. Ile chemba imeziba na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa mpaka hivi sasa, maji hayo yamekuwa tatizo na isitoshe eneo hill kuna shule sasa sijui wanafunzi wanasoma vipi na hiyo harufu Kali inayotoka maeneo hayo.
Ukiachana na hapo pia kuna chemba nyingine ipo maeneo ya Forest ya zamani karibu na Hospitali ya Mbeya Surgical iliyo mkabala na chuo cha CUOM hii ndiyo balaa maana ipo karibu na makazi ya watu.
Mwanongwa nawakumbusha tu kuwa jiji letu linanukaaaaa