Idara ya Uhamiaji yasema haijazuia kutoa Visa kwa Wageni

Idara ya Uhamiaji yasema haijazuia kutoa Visa kwa Wageni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-11-06 at 08.27.43_fdb80ec6.jpg

YAH: UTOAJI WA HUDUMA YA VISA ON ARRIVAL KUINGIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuwajulisha wageni na wadau wote kuwa haijasitisha utoaji wa Visa kwa wageni kwenye vituo vya kuingilia na kutoka nchini.

Hata hivyo, Idara ya Uhamiaji Tanzania inashauri wageni wote ambao wanapenda kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni mbalimbali kuomba Visa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo wa Visa mtandao (e-Visa) Tanzania eVisa - Welcome. Kuomba Visa kabla ya kuingia nchini mgeni anakuwa na uhakika wa safari yake na hupunguza msongamano na muda wa kuhudumiwa wakati wa kuingia nchini.

Aidha, Idara ya Uhamiaji Tanzania inawahakikishia kuwa inaendelea kutoa huduma bora zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa kwa wageni wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.

SSI. Paul Mselle
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Tanzania.
 
Mwezi mmoja uliopita nilimuombea rafiki yangu visa anaeishi Nigeria si mara yakwanza kumuombea nahuwa anakuja ila this time ilishindikana huwa naomba kupitia online nimelipia gharama za visa majibu yamekuja reject nikaomba mara yapili malipo ya application wanachukua lakini majibu yanakuja reject nimeamua kuwa mpole
 
Back
Top Bottom