KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Naomba kuwasilisha kero sugu iliyopo katika Halmashauri ya Nachingwea upande wa Idara ya Utumishi, kumekuwa na mikingamo mingi na mazingira tata katika utoaji wa barua za uthibitisho na barua za ajira kwa sisi Watumishi wa Serikalini.
Hizi barua hazitolewi kwa wakati na mpaka sasa, kawaida Mtumishi unapofanya kazi na kumaliza mwaka mmoja unatakiwa kupata barua ya uthibitisho kazini.
Sisi tulioajiriwa katika Halmashauri hii upande wa Elimu na Afya hatujapata barua zetu licha ya kuwa tumefanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na miezi sita.
Kila tukienda kuulizia tutaambiwa wako ‘busy na uchaguzi’ hii ni sawa kweli?
Tumeuliza wenzetu ambao tuliwakuta kwenye kazi wametuambia changamoto hii ipo miaka yote, wanachelewesha bila kuwa na sababu za msingi na wala wasisingizie kuwa kuna Uchaguzi, tunahisi kuna mazingira ya rushwa ili kupata barua hizo.
Ujumbe huu ufike Utumishi makao makuu wajue kuwa kuna watu wanatufanyia ndivyo sivyo, mbona wenzetu kutoka maeneo mengine wao tunasikia wamepata barua?
Kukosekana kwa barua hizo kunatunyima haki ya kujitambua kuwa na sisis ni sehemu ya Watumishi rasmi na pia hatuwezi kupata mahitaji mengine ya msingi kama mkopo, tunaomba kilio chetu kisikilizwe.