Idd Makengo anatunga stori na kuwapumbaza watu hasa wanawake

Idd Makengo anatunga stori na kuwapumbaza watu hasa wanawake

Riskytaker

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2024
Posts
568
Reaction score
2,522
Ukisoma visa ya Idd Makengo, utagundua 99% ni visa vya kutunga. Yaani anatengeneza mtiririko wa matukio bandia ili apate likes na comments akuze page yake.

Sasa kwenye comments unakutana na wanawake hata 2000. Wanakoment kwa hisia, kumbe ni hadithi za kutunga.
 
ukisoma visa ya idi makengo utagundua 99% ni visa vya kutunga .

yaani anatengeneza mtiririko wa matukio bandia ili apate likes na comments akuze page yake

sasa kwenye comments unakutana na wanawake hata 2000. wanakoment kwa hisia kumbe ni hadithi za kutunga
Ndio ubora wa mwandishi kugusa hisia za wasomaji.

Kwani anaandika kuhusu nini?
 
Wanawake wana aina zao za masimulizi ambayo huyataka. Mama yangu akianza simulia habari za kanisani au Radio Maria sisikilizi. Wadogo zangu wa kike wana masimulizi yao ambayo siyaelewi kabisa.

Hata sisi wa kiume tukizungumzia mpira wa kike wanaona tunapoteza muda. Kwahiyo mwandishi ana niche yake, mfano mimi siwezi sikiliza The Strory Book sijui iko Clouds au Wasafi. Ni ya watu wenye IQ ndogo wanatakiwa wasikie zile conspiracies.
 
ukisoma visa ya idi makengo utagundua 99% ni visa vya kutunga .

yaani anatengeneza mtiririko wa matukio bandia ili apate likes na comments akuze page yake

sasa kwenye comments unakutana na wanawake hata 2000. wanakoment kwa hisia kumbe ni hadithi za kutunga
Si ndio maana ya Fasihi, kwani Movie zote unazoangalia ni za kweli?
 
Tatizo la watu wa humu mnadhani kila mtu anamtumia Facebook!

Ilipaswa utueleze huyo Idd Makengo ni nani na simulizi zake zinahusu Nini Ili na sisi tusiyemfahamu tujue tunachangia Nini!
 
Idd makengo yupo kwenye vinywa vya wanawake kama mwamposa..halafu Kila story muhusika ndani yake anaonekana kusifia vitabu vyake.."oh basi mme wangu nlivoachana .nae Maisha YAKAWA magumu so unakumbuka nlikutafuta ukanishauri ninunue kitabu chako Cha biashara 50.kwakweli nimefungua duka kubwa sana..kitabu chako minisidia mno""
Nyingine"Mahusinao yangu yalivyoyumba nkatafuta kitabu chako cha hakuna kuachwaachwa.,sahivi ndoa yangu umerudi Ina furaha kama zamani.

Hata hivo ni marketing strategies zake tu.
 
ukisoma visa ya idi makengo utagundua 99% ni visa vya kutunga .

yaani anatengeneza mtiririko wa matukio bandia ili apate likes na comments akuze page yake

sasa kwenye comments unakutana na wanawake hata 2000. wanakoment kwa hisia kumbe ni hadithi za kutunga
Iddi Makengo ndo nani!? Unaandika kama vile kila mtu anamfahamu!!!
 
Hata mimi ni good storyteller sema ndio hivyo.
 
ukisoma visa ya idi makengo utagundua 99% ni visa vya kutunga .

yaani anatengeneza mtiririko wa matukio bandia ili apate likes na comments akuze page yake

sasa kwenye comments unakutana na wanawake hata 2000. wanakoment kwa hisia kumbe ni hadithi za kutunga
Nilishawahi kuandika hii sehemu.

Jamaa ma story yake hayana uhalisia
 
Back
Top Bottom