Idd Simba huru,Mahakama yamfutia mashtaka!

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA), Idd Simba,Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza(CCM), Salum Mwaking’inda,Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi. Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru.
 
weeeee hilo tulilitengemea tulio wengi, sheria zipo kwa ajili ya masikini 2!
 
...ule mkwara wa dhamana sijui ya bilioni moja,nilijua jamaa lazima ashinde kesi...
 
Ili kuziba vizabizabina inabidi wafungue kesi kuishitaki serikali kwa udhalilishaji na kuwatia aibu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…