Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kuna mtu kaniuliza ni nani Iddi Faiz Mafungo?
Maswali kwangu yanakuwa mengi mno kuhusu historia ya TANU na Mwalimu Julius Nyerere kiasi naelemewa.
Muulizaji angeweza kuingia Google angemsoma lakini naona si adabu kumwelekeza huko.
Nimeamua kuweka picha ya Iddi Faiz Mafungo hapa na maelezo yake kidogo kwa faida yetu sote.
Huyo aliyesimama mkono wa kulia wa Nyerere ndiye Iddi Faiz Mafungo.
Hapo wapo uwanja wa ndege wanamsindikiza Nyerere safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955.
Iddi Faiz alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na pia Mweka Hazina wa TANU.
Kwa ajili ya nafasi hizi mbili alizoshika ndiyo akachaguliwa kuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere UNO.