Idea ya biashara: Kutengeneza vibanda vya wamachinga na kuvipangisha

Idea ya biashara: Kutengeneza vibanda vya wamachinga na kuvipangisha

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Wakuu nina idea ya kitengeneza vibanda vya wamachinga na kuvipangisha. Vibanda hivyo nitaviweka pembezoni mwa barabara zote kubwa zilizopo mjini..kuanzia Shekilango, Sinza, Goba, Mbezi n.k

Naomba kama kuna mwenye mchango wa mawazo.

1625122662769.png

 
Wazo zuri, lakini kuviweka pembeni mwa barabara utakuwa umeboresha tu vilivyopo. ungevijenga kwenye eneo moja linalofikika kirahisi bila kuwa na mtazamo wa mkusanyiko wa watu.... mfano uwanja wa maonyesho saba saba, uwanja wa mpira ...kwa mkapa, uwanja wa ndege n.k.
 
Ni wazo zuri ila kama una sehemu ya kiwanja kikubwa ni bora zaidi tena unafanya baadhi ya siku tu ili kupungiza kadhia kwa watembeaji wa miguu na halmashauri pia

Hawachelewi kupita pita
 
Wazo zuri ila machinga sio watu wazuri sana kama unavyofikiria
 
Wakuu nina idea ya kitengeza vibanda vya wamachinga na kuvipangisha. Vibanda hivyo ntaviweka pembezoni mwa barabara zote kubwa zilizopo mjini..kuanzia Shekilango, Sinza, Goba, mbezi n.k naomba kama kuna mwenye mchango wa mawaxo
Wazo zuri lakini humo pembezoni mwa barabara lazima tu utagombana na halimashauri!!labda kama sio kwenye hifadhi ya barabara, ambacho ni kitu kigumu!!
 
Back
Top Bottom