Idea ya Kuanzisha chuo kinachotoa Certificate ya madini na baadae Diploma

jashmoe32

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
1,089
Reaction score
424
Habari wanajamii,

Nlikua na idea ya kuanzisha chuo kinachotoa Certificate na baadae Diploma ya Mineral Processing/Metallurgy hapa Tanzania. Kwa sasa hivi,chuo yabidi kifate wanafunzi na kwa nchi yetu vyuo vinavotoa certificate ya hiyo kitu ni vichache sana, na mimi nlikua na wazo la kua kati ya hao wachache.

Mimi nina knowledge ya Mineral Processing/Metallurgy na nimespecialise mostly on Gold, Copper, Coal na other Base Metals na pia haitokua ngumu kujifunza kuhusu processing ya Almasi. Nlikua na idea kama naweza kupata mtu ambae yuko good katika Mining Engineering na Geology ili tuungane kwa pamoja mana ni vizuri kila mtu atumie skills zake na si kulazimisha kitu ambacho si cha kwako ili udanganye watoto wa watu.

Swali langu ni je, hiki chuo mnaona bora kianzishwe Mwanza au Shinyanga au mnaona mkoa gani utafaa?Dar haitofaa kwa sababu watu wengi hawako interested na mambo ya madini kama Mwanza, Shinyanga au maeneo yote yenye Mineral deposits.

Ntashukuru sana kwa mchango wenu mana nia yetu sote ni tusonge mbele na tufanikiwe katika kujiendeleza vijana. Najua mwanzo ni mgumu ila kwa kudra za Mwenyezi Mungu,naamini ataniwezesha kwa yote.

Nahitaji mchango wenu wa mawazo na hata kama mtu anaweza kujitoleo eneo ili tuweze kuanza taratibu na tujue tutafikia wapi.

Ntashukuru kwa ushirikiano wenu.

Wenu

Jashmoe
 
Hongera !! Na idea yako ibarikiwe...
Mimi sina ujuzi wa Madini, Uwezo wa kifedha sina shaka nipo imara , Pili nina kitalu sehemu fulani!! Sasa makubaliano yetu yawejee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…