Idris asema Wema kutumia Tsh milioni 4.8 kwa ajili ya nywele kwa mwezi ni hadhi yake

Idris asema Wema kutumia Tsh milioni 4.8 kwa ajili ya nywele kwa mwezi ni hadhi yake

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
xWema.jpg.pagespeed.ic._JoTbWrGkB.webp


Wema na Idris katika pozi

Aidha katika kauli nyingine ambayo Wema aliitoa mapema mwaka huu, alisema anatumia Sh 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Idris Sultan ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother 2014, amesema haoni tatizo kwa mpenzi wake huyo kuwa namataumizi makubwa kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtafutaji.

“Kwa level yake anafaa, kila mtu na level yake,” alisema Idris. “Kwa hiyo nina maanisha kila mtu ana thamani yake, na kila siku hadhi ya maisha yake inapanda na pia anafanya kazi ndiyo maana anafikia katika level hiyo,”

Pia Idris alisema watu wanatakiwa kutambua kwamba jinsi uchumi wa mtu binafsi unavyokuwa basi pia na maisha yake hudabilika pamoja na muonekano.
 
Sijapenda kabisa kuwa Wa kwanza kuchangiaa huu uzii...nimelazimishwaaa
 
hivi idris hana mama au baba au ndugu wa damu?
Hawezi kukosa, kama anao kweli j wanampenda kwa dhati nahisi kale kamsemo "mkaid hafaid mpaka siku ya idi" kanahusika vya kutosha
 
Waachen bax kila mtu na life style yke ghraaaaaa!!!!!ye kaona urembo ni bora kuliko nyumba km mpoki aliivyoona gari ni bora kulko nymba(anatania))!!
 
Hawezi kukosa, kama anao kweli j wanampenda kwa dhati nahisi kale kamsemo "mkaid hafaid mpaka siku ya idi" kanahusika vya kutosha
Na ndo mana anaakisi maisha ya wanaume wa dar! ashakum si matusi
 
Kweli Idris nae ni cm fake inayotakiwa kuzimwa na TCRA.Anaacha kumshauri huyo bibi yake anunue kiwanja ajenge. Anamsifia kuvaa nywele fake. Umri unazidi kumpita mkono, akija kustuka hawezi miliki hata bajaj. Na hizo ngozi na mkorogo zinavyowahi kuchakaa. Bila make up hatoki nje.
 
Ndo shida ya kudate na watoto. Sasa ndo maneno gani ayo ya kitoto anayoongea idris. Nywele za 4M halafu mradi wa kueleweka hamna. Upuuzi mtupu, kwel Tanzania tuna vivutio vingi
 
wanaume wa dar
Hahahahahaaaa hao ndio wanaume wa dar, wanakuambi eti dar kuna mzunguko wa hela, so hata ukikaa kijiweni unacheza draft na kunywa kahawa na kashata pesa inakuzungukia tu. Wakazi wa dar wananichekeshaga
 
Back
Top Bottom