Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
๐๐ฑ๐ฟ๐ถ๐๐๐ฎ ๐๐๐ฒ๐๐ฒ ni mchezaji wa klabu ya mpira wa miguu ya Paris Saint Germain (PSG) aliyekataa kuvaa jezi ya timu yake ambayo kwa upande wa namba ilikuwa imeandikwa rangi zenye kuashiria mahusiano haramu ya jinsia moja na watu waliobadili jinsia kwa pamoja wanajitambulisha kama LGBT+.
Hivi karibuni ametoa kauli kufuatia sakata lake hilo la kuonekana kwamba anadharau alama hiyo na kuikataa kabisa akisema: "Nipo tayari kuondoka Ufaransa (na kuachana na klabu ya PSG) ila sitaomba radhi (wala kutaka msamaha). Nafahamu misingi ya Imani yangu, sihofii kupoteza Mkataba au Umaarufu wangu hapa Ulaya, nipo tayari kurudi nyumbani (Afrika)".
Hayo yamekuja baada ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Ufaransa kumtaka aombe radhi kwa kitendo hiko cha kiimani alichokifanya.
PIA SOMA
- Akacha mechi kwasababu hataki kuunga mkono vitendo vya kishoga