IEBC commissioners agree to exit but want 'dignified' pay deal

Nadhani tofauti ya wakenya na watz iko wazi, wao hawakulalamika bali walitia shinikizo kubwa wakiwatumia wanasiasa, wasomi wabobezi wa sheria na NGO'S hadi IEBCC ikasalimu amri kwa maslahi mapana ya mama Kenya. Tanzania kila mtu analalamika tu, sasa kweli tutapata mabadiliko kwa malalamiko?? we should not lament but rather pressurize........
 
Hata Uhuru Kenyatta amechangia sana,maana walipopeleka sheria kandamizi ya mitandao aliirudisha Bungeni akawauliza kama kweli wamejadili nankuona impact ya kuwafunga waandishi wa habari na wakenya midomo!Akawaomba warudie upya kyusoma muswada na kuujadili kabla hajausaini na hapa kwetu je?Ndiyo tuliona mahali pa kuwafungia midomo watanzania na wapinzani.
 
HATIMAYE KENYA WAFAULU KUIONDOA TUME MBOVU YA UCHAGUZI.
••••
•••

Makamishna wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC wamekubali kuondoka ofisini kwa masharti ya kulipwa mishahara na marupurupu yao,hatu aitakayomaliza mvutano wa muda mrefu ulioanzishwa na wanasiasa wa upinzani wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi.
Hatua hii inayotajwa kuwa ya kihistoria wakenya wanaizungumziaje?mataifa jirani za Kenya wanajifunza nini?Je ni uamuzi sahihi?Kuondoka kwao kutatoa hakikisho la uchaguzi huru na haki mwakani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…