IEBC yakutana kujadili uchaguzi ujao

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Tume ya IEBC inakutana kwa mara ya kwanza tangu mahakama ya juu iagize marudio ya uchaguzi wa urais mnamo ijumaa wiki iliyopita. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kutenga tarehe ya uchaguzi huo mpya ambao sharti uandaliwe katika muda wa siku 60 zijazo. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alikuwa amesema kwamba mkutano huo utapendekeza mabadiliko yatakayotekelezwa katika makao makuu ya tume hiyo huku ikijiandaa kwa marudio ya uchaguzi wa urais. Chebukati alimtaka mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuchunguza na kumshtaki afisa yeyote wa tume hiyo ambaye huenda alikiuka sheria wakati wa uchaguzi mkuu mwezi jana. Chebukati alisema yeyote atakayepatikana alikiuka kanuni za uchaguzi na kusababisha kubatilishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais lazima awajibike.
 
Kwetu hapa Lubuva angeweza kutamka maneno ya huyu msabato?! Angalau wenzetu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wanajaribu kuwa wazi kidogo. Pamoja na hayo ilitakiwa kubadilishwa kidogo ili ikidhi haja

Cairo's
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…