Sekta ya benki ni mojawapo ya sekta zinazofanya vizuri katika Dar es Salaam Stock Exchange ikiwa na taasisi kama CRDB Bank Plc, NMB Bank Plc, MKCB, MBP na DCB Commercial Bank Plc.
Lakini pia ni sekta inayosimamiwa kwa ukaribu mkubwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa sababu inahusisha fedha za wananchi.
🏦 Biashara Kuu ya Benki Ni Nini?
Kwa lugha rahisi, biashara ya benki ni:
Kukusanya fedha (deposits) kutoka kwa wateja na kukopesha fedha hizo kwa riba ili kupata faida.
Hivyo chanzo kikuu cha mapato ya benki ni:
1️⃣ Interest Income (Mapato ya Riba)
Haya ndiyo mapato makubwa zaidi — yanatokana na mikopo inayotolewa kwa watu binafsi, biashara na taasisi.
Hivyo basi, katika uchambuzi wa benki, ni muhimu kuona:
✓ Je, mikopo inaongezeka?
✓ Je, mapato ya riba yanakua mwaka hadi mwaka?
✍️ Ukuaji hapa unaonyesha biashara kuu ya benki ina afya.
2️⃣ Non-Interest Income (Mapato Yasiyotokana na Riba)
✓ Mbali na mikopo, benki hupata mapato kutoka:
✓ Ada za akaunti (account maintenance fees)
✓ Ada za miamala na huduma (fees & commissions)
✓ Biashara ya fedha za kigeni (forex trading)
✓ Uwekezaji kama hati fungani za serikali au hisa
✍️ Benki bora huwa na interest income kubwa kuliko non-interest income.
📊 Vipimo Muhimu vya Kuangalia Ubora wa Benki
Kuna vipimo vingi vya kuchambua benki, lakini viwili ni muhimu sana kwa mwekezaji:
✅ Non-Performing Loans (NPL)
Hiki hupima ubora wa mikopo — yaani mikopo ambayo haijalipwa kwa muda uliokubaliwa.
Kadri NPL inavyokuwa ndogo:
👉 Ndiyo benki ilivyo salama zaidi.
✅ Cost to Income Ratio
Hiki hupima:
Je, benki inatumia gharama kiasi gani kuzalisha mapato?
Kadri ratio inavyokuwa ndogo:
👉 Ndiyo benki inavyokuwa na ufanisi zaidi katika matumizi.
NB: Tutaangazia kila moja kwa undani zaidi katika masomo yajayo.
📌 Swali la Leo:
Kutokana na Somo la Leo, ni benki gani unaona ina potential ya kufanya vizuri sana baadae ukilinganisha na inavyofanya sasa?
Kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji, karibu kwa ajili ya Madarasa na Mentorship: 0763721523 (whatsApp).