Tatizo sio boss wala sio wewe tatizo ni namna ulivojipa umuhimu kwenye hiyo kazi au ofisi. Yapaswa kutambua ata ukifa leo baada ya siku chache kila mtu maisha lazima yasongee awe mume, mke, mtoto au Rais wa nchi.
Siku ukipotea kama Ben Sanane maisha bado yatasonga, wewe fanya unachoweza hapa duniani. Gusa maisha ya watu, saidia wengine ukitambua hata usipowasaidia wataendelea kuwepo na sio wewe uliowasaidia kufika apo.
Tumia akili sana kuliko hisia, sio kila mara unasema ukweli muda mwingine unapindisha kwa manufaa mapana ya umma. Tambua hakuna mtu mwenye haki ya kuthamini umuhimu wako popote anaweza akakudharau akanyanyapaa kulingana atakavoona inampendeza.
Muhimu fanya ulichofuata kama ni kazi piga kazi, kama ni kazi plus heshima lipa watu wakuamudu wakuite Masiha, Malkia,.......... Maisha ni akili na akili ni kile kinachobaki kichwani kwako baada ya kutoa vyote ulivyofundishwaa by Albert Einstein et al.,