Wadau ningependa kusikia maoni yenu.... nauliza hiviii.... kama ungepata nafasi ya kuibadili Tanzania ya leo ungefanya nini?...
Mkuu,
Unapoibuka ghafla na swali kama hili bila hata kuwa na utangulizi, unakuwapo unakosea.
Wewe anza kwa kutuambia kwamba una mawazo kuhusu kuibadili Tanzania ya leo halafu sisi tutafuatia.
Ila kwa kuendelea kukukaribisha, mimi nina maoni yafuatayo:
1. Ntaitisha kura ya maoni ya kuibadili katiba ya Tanzania, iendane na zama za sasa zenye mambo kama kuwa na wagombea ambao wameishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa, wenye umri usiozidi miaka 50 na si chini ya miaka 35, kupewa nafasi ya kuleta ujuzi na uzoefu katika ardhi ya nchi yao.
2. Ntabadili mfumo wa serikali ili kuwa na serikali za mitaa zenye kubuni na kupanga mipango yake bila kuingiliwa na serikali kuu isipokuwa kwa masuala ya kuchagua madiwani na meya ambapo itabidi pawepo na wagombea binafsi na pia meya kuchaguliwa na wananchi badala ya baraza la madiwani.
Hii inatoa nafasi kwa wananchi wote kuwa na nafasi ya kuchaguliwa kuongoza mkoa au wilaya.
3. Ntazifanzia mabadiliko sekta za Elimu, Afya, Jamii, Uhamiaji kwa kuwapa kazi hio wataalamu waliosomea mambo hayo ambao wapo tu wanasoma magazeti kila siku asubuhi maofisini. Ntataka waje na mawazo yao ingawa na mimi ntakuwa na mawazo yangu ambayo ni kama ifuatavo:
(a) Katika elimu ntapenda nione kila mtoto wa kitanzania anaefikisha umri wa mwaka mmoja, anaanza shule ya awali na walimu wanakuwa wapo wameandaliwa. Pia kila mtoto ambae amefikisha umri wa kuanza darasa la kwanza anafanza hivo na ntataka mtoto yoyote akifikisha umri wa miaka 14 tayari anajua kila kitu kuanzia kusoma,kuandika na ntatilia mkazo katika hisabati na Kiingereza.
Ikumbukwe kuwa baadhi ya watoto wanapomaliza shule ya msingi bado wanakuwa ni mambumbumbu. Kwa hio kuanzia umri wa miaka 14 hadi 19 mtoto yoyote yule tayari anakuwa amekwishajulikana ana kipaji gani na ni namna gani ya kumuendeleza iwe katika sayansi, ufundi na mengine kwa hio inabaki kumpa nafasi ya kuwa mtaalam katika fani yake kupitia vyuo na shule maalum.
(b) Katika sekta ya Afya ntahakikisha kwamba madaktari wote waliosoma nje ya nchi wanapokuja nyumbani likizo basi tunahitaji msaada wao wa kitaaluma hasa katika maeneo ambayo kumuona daktari ni taabu. Kwa mfano daktari anaishi na kufanza kazi Ujerumani lakini kazaliwa Kisiju Pwani, basi hata kama ana nyumba mbezi tutampa kiwanja ajenge Kisiju Pwani ili awe karibu na wananchi wenzie. Pia wale ambao wamestaafu basi serikali itaingia mkataba nao ili kusadia jamii za watanzania.
(c) Sekta ya jamii, hili ni tatizo mahala popote duniani na hata Marekani ambako wameendelea ni kwamba kama hukuweka akiba ulipokuwa unafanza kazi basi utakuwa na matatizo pale utapohitaji msaada (nafikiri umetazama movie ya John Q).
Kwa hio ntahakikisha kila mtu ambae amejiajiri anachangia mfuko wa pensheni ili fwedha zile zimsaidie pale anapopata dharura na anapostaafu kufanza kazi. Kwa maana moja au ingine ntajitahidi kubuni njia mbalimbali za kuwawezesha watu kufanza kazi na kupata revenue kupitia kodi mbalimbali.
(d)Kuhusu sekta ya uhamiaji ntahakikisha kwamba kila mtoto anaezaliwa katika ardhi ya Tanzania anajulikana kwa kuweka kumbukumbu ambayo itasaidia ku-balance allocation ya resources kama elimu na afya kwa mtoto huyo (nafikiri unanifahamu hapo). hapa ntakuwa najaribu kuzuia raia wasio watanzania kufaidi mambo ambayo ni kwa watanzania tu isipokuwa kama baba na mama au mmoja wao ana uraia wa Tanzania.
Hapa namaanisha kwamba watu wote wasio raia wa Tanzania wanakuwa "second" kwa watanzania katika kupata "resources" kama elimu, ajira, makazi na kadhalika.
Hayo ni baadhi ya maeneo ambayo ninaona yahahitaji mabadiliko ya haraka ingawa kuna maeneo mengine kama biashara na viwanda, usafiri na usafirishaji ambayo ningeyatia katika awamu ingine tuchukulie ninapewa awamu mbili.
Ntaelezea namna ya kubadili maeneo haya kadiri tunavoendela kujadiliana.
NB:
Mimi sio mwanasiasa lakini napenda mabadiliko yawe ya kisayansi zaidi.
Ahsante.