Ifahamu AIS (Automatic Identification System)

Ifahamu AIS (Automatic Identification System)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
AIS-Automatic Identification System hiki ni kifaa kinachotumika kutoa taarifa za meli na huwa kinafungwa katika meli au mnara wa mawasiliano au kuongozea meli (Vessel Traffic Services).

Ufanyaji kazi wake
AIS imeunganishwa na GPS, Satellite, mfumo wa mawasiliano wa VHF, transponder na navigation sensors.

Taarifa upatazo kutoka AIS
Speed ya meli,Uelekeo,Eneo meli ilipo, Jina la meli,Ukubwa wa meli, Meli zilizo jirani yako.

images.jpeg

1.Kupunguza ajali za meli kugongana
Kifaa hiki hutumika melini na nchi kavu kimekuwa muhimu kusaidia kupunguza ajali za kugongana meli sababu uonyesha meli zilizo karibu nawe kwa kukupa taarifa ya uelekeo, umbali na eneo la meli nyingine.

2.Kusaidia kuongoza makundi ya meli

3.Ulinzi wa bahari

Meli yoyote ikiwasha hiki kifaa lazima meli zilizokaribu yake zitapata taarifa zake na wale wa mnara wa mawasiliano wataiona kisha kuangalia hiyo meli inafanya nini.

4.Kisaidia kuongoza meli
AIS huonyesha taarifa za eneo husika kama maboya na alama nyingine katika ramani.

5.Uokoaji na utafutaji makini
AIS usaidia kutupa taarifa sahihi wapi chombo kipo,uelekeo pia mfumo wa utafutaji na uokozi wa ndege umeunganishwa na meli hivyo kwa taarifa hizo kazi urahisishwa.

6.Uchunguzi wa ajali
AIS hutumika wakati wa uchunguzi wa ajali ili kujua taarifa za meli ilipokuwa,speed, uelekeo na taarifa hizo uonekana vizuri kwenye Black Box.

Meli zinazotakiwa kuwa na kifaa hiki
Shirika usimamiaji wa meli duniani linataka meli zote kuanzia tani 300,meli zote za masafa na abiria kuwa na hiki kifaa.

Nyongeza;Maharamia wengi mfano wale wa Somalia walikuwa wanakuwa na hiki kifaa hivyo walikuwa wanapata taarifa za meli zipitazo pwani yao.

Ndio maana walikuwa wakijua meli imetoka wapi, ipo eneo gani, speed yake hivyo hata ukiongeza speed wao waona na hutumia fiber boat kufukuzia ili kupata meli.

Kifaa hiki pia huzimwa pale meli zinazofanya uvuvi haramu kwenye nchi nyingine ili wasionekane. Ila ukikamatwa na mamlaka kesi yake ni kubwa.

AIS inasaidia sana kujua baina ya meli na meli.
Picha ya kifaa hiki cha AIS
 
Shukran mkuu huwa nakufatilia nafanya biashara za uvuvi ziwa victoria nikija dar nitakutafuta unifumbue kuhusu boti ndogo ndogo niwekeze huko badala ya mitumbwi ya injini ya kuchonga.
 
Sawa mkuu, panapo majaliwa hata mimi nina mpango wa kuja huko naweza nikakucheki nikiwa Mwanza.
 
Back
Top Bottom