Ifahamu biashara ya Spea za Pikipiki na Bajaji (Sehemu ya Tano)

Jvei

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
42
Reaction score
69
JINSI YA KUSIMAMIA NA KUENDESHA BIASHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI NA BAJAJI.
⚙Watu wengi wanatamani sana kufanya  Biasha hii, laikini hawajui jinsi gani wanaweza kusimamia biashara yao ili iweze Kukua na kuleta manufaa na faida.
Suala hili limekuwa changamoto zaidi kwa wale wenye shughuli/kazi/biashara zaidi ya moja lakini wanatamani kufanya biashara ya spea ili kuongeza kipato chao.
Njia zinazotumika kwaajili ya usimamizi wa biashara ni njia mbili:
1. Njia ya kawaida/kitamaduni
2. Njia ya kidigitali
⚙Njia ya Kawaida
Njia ya kawaida/asili hii huhusisha ku kontrol Ufungashaji wa bidhaa, mauzo, mapato na matumizi kwenye biashara ya spea.
Njia hii huhusisha ku record kila bidhaa inayoingia kama stock na kila bidhaa inayotoka, mauzo yote, mapato na matumizi pia. Njia hii hulenga kuweka kumbukumbu sahihi za mwenendo wa biashara kwa mmiliki wa biashara.
Njia hii huenda Sambamba na msemo "mali bila daftari, Huisha bila habari".
Ni wazi kwamba njia hii ndio hutumika zaidi kwenye biashara nyingi. Na husaidia sana kutunza kumbukumbu muhimu za biashara hivyo kufanya ukaguzi wa mwenendo wa biashara kuwa rahisi.

⚙Njia ya kidigital
Njia hii huhusisha mifumo ya kisasa inayopakuliwa kwenye simu au compyuta.
Dhumuni lake ni sawa na nile la njia ya asili, japo mifumo ya kidigitali hurahisisha zaidi kwani hutunza kumbukumbu yenyewe ukishaingiza tu mauzo, hukuambia faida ni kiasi gani, stock ya bidhaa hiyo imebaki kiasi gani. Here Hurekodi mauzo ya saa, wiki, mwezi na hata mwaka na kutoa taarifa ya mapato, matumizi, garama za uendeshaji, faida, hasara n.k automatically. Kinachohitajika ni kujaza tu taarifa kwenye program hiyo kama inavyotakiwa.
Program hizo ni kama vile; EzeAccounting, Linda Pesa, Duka Manager n.k. (tutazijadili zaidi wakati mwingine)
Njia hii kama ilivyo njia ya kawaida, zote zinahitaji mtu makini kuweza kujaza taarifa za mwenendo wa biashara kwa uaminifu na umakini mkubwa.
Pia njia zote mbili zinahitaji usimamizi, yaani zinahitaji awepo mtu anayeweza kujaza taarifa. Awe mmiliki wa biashara mwenyewe au mfanyakazi wake.
Kwenye Dhana ya usimamizi kama ni mfanyakazi ndio huingiza data, basi mmiliki unapaswa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha taarida zinazoingizwa ni sahihi.

Mimi ni Muajiriwa, je ninaweza kufanya biashara ya spea za pikipiki bila kuathiri kazi yangu?
Ndio, kila mmoja mwenye malengo na kiuya kufanya biashara kuongeza kipato chake anaweza kufanya biashara hii na ikampa faida nzuri kabisa bila kuathiri shughuli zake nyingine.
Hapa unaweza kutumia njia zifuatazo:

1. Ajiri mfanyakazi akusaidie kuuza duka lako, hapa utatakiwa kutafuta mtu unayemuamini na utamuajiri na kumlipa kwa Kadri mtakavyo kubaliana. Hata hivyo, uangalizi wa karibu na ukaguzi unahitajika ili kuhakikisha hakuna hasara wa upotevu wa mapato kwenye biashara yako.

2. Kufanya Ubia/ partnership;
Kama unataka kuanza biashara hii ya spea za pikipiki na bajaji lakini huna muda wa kutosha kusimamia biashara yako, basi unaweza kuamua kufanya partnership na mtu mwenye ujuzi, elimu na utaalamu wa biashara hii na wewe ukatoa sehemu ya mtaji ili kuwezesha biashara hii kwa Kadri mtakavyo kubaliana.
Hata hivyo kwa watu wenye mitaji mikubwa (35m+) njia hii ni bora sana. Itakurahisishia namna ya usimamizi, kwani mkiwa shirika, mmiliki mwenza wa biashara huwa na umakini kwenye kuilinda biashara kuliko mfanyakazi.
Partnership inaweza kuwa kwa makubaliano maalum, ikiwa kama utakuwa huna muda kabisa wa kuhusika na biashara, basi mnaweza kukubaliana kiwango maalumu amabacho mmiliki mwenza atatakiwa kukupatia kama faida kila baada ya muda fulani.
Kwenye njia hii Kuna ofa, kwa wale wanaotaka kufanya biashara hii Dar es salaam na wanaweza kufanya partnership, basi habari njema ni kwamba, Kuna watu wenye connections zote za spea, suppliers, ujuzi, maeneo mazuri na mafundi lakini hawana mtaji/mitaji yao ni midogo hivyo mnaweza kujadili mkaona namna ya kufanya biashara kwa pamoja na mkafaidika nyote.

Je, biashara ya spea za pikipiki na bajaji ni uwekezaji wa kuaminika?
Ndio. Bila Shaka yotote.
Biashara ya spea za pikipiki kwa hapa Tanzania, na Afrika Mashariki yote ni biashara inayokua kwa kasi, hivyo uwekezaji wake ni wa uhakika sana.
Kwa Kadri unavyoingia na mtaji mkubwa ndivyo hukupatia return kubwa na ya haraka. Ndio, biashara hii wastani wake wa chini ni kukupatia faida sawa na mtaji wako ndani ya mwaka mmoja.
Mfano: Ukiwa na mtaji wa 20m, basi biashara hii ina uwezo kabisa wa kukupatia 20m+ kama faida ndani ya mwaka mmoja.

Je, nikitaka kufanya biashara hii nitapata wapi muongozo na mzigo?
Moja kati ya dhumuni la maandiko haya, ni kuwaletea fursa kila mmoja. Kutoa elimu, na muongozo wa kibiashara.
Hivyo kwa yoyote anayehitaji kufanya biashara hii ya spea za pikipiki na bajaji popote pale Tanzania na hata nchi jirani anaweza kuwasiliana nami.
Ukiwa unataka kufanya biashara ya spea za pikipiki kwa Jumla na rejareja, rejareja ama jumla peke yake basi karibu sana. Utapata Maarifa, Ushauri na Usimamizi.
 

Attachments

  • IMG-20250811-WA0014.jpg
    690.4 KB · Views: 59
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…