Ifahamu Biashara yenye Utajiri ya 'Real Estate'

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
779
Reaction score
1,269
Wakuu, habari ya Jumapili. Hope wote mpo vizuri. Kwa wale wenye changamoto za hapa na pale, poleni, Mungu awe pamoja nanyi katika kipindi hiki.

Kama ada, imekuwa ni utamaduni wa ku-share kile ambacho tumekivuna kwenye jamii, vitabu na uzoefu. Leo nataka niwashirikishe wadau ili kupanua uelewa wetu katika hii biashara ya 'Real Estate',

Biashara yenye utajiri mkubwa, biashara ambayo tajiri yoyote unayemfahamu na unayemsikia amewekeza huko. Labda ningeangaliza tu, kwakuwa nimesema kuwa tajiri yoyote amewekeza kwenye hii biashara, basi masikini au watu wa tabaka la kati hawawezi kuwekeza hapa, la hasha.

This is business for everyone, nasisitiza mtu wa tabaka la chini, la kati na la juu kiuchumi unaweza kufanya hii biashara.

Biashara ya 'Real Estate' ni biashara ya mali, hasa majengo na ardhi yake pamoja na ardhi na vilivyomo. Ni biashara ya kununua na kupangisha au kuuza hivyo nilivyovitaja hapo juu. Ni biashara ambayo unahusisha kutumia ardhi yako na vilivyomo na majengo (nyumba za kupanga, nyumba za kuishi, stoo,majengo ya ofisi, majengo unayoweza kutumia kama hoteli, gereji, kiwanda, malls n.k)

Kwa watu wa kipato cha chini na kati kwa sehemu kubwa wanaweza kumudu kumiliki 'Real Estate' za Makazi na Za Kibiashara. Aina ya 3 ya 'Real Estate' ambayo inahusisha viwanda, migodi n.k inaweza kusubiri mtaji kuongezeka kwa wewe mfanyabiashara unayeanza chini.

Unaweza kuwekeza katika Biashara ya 'Real Estate' kwa namna zifuatazo;-

1. Nunua hisa katika kampuni inayojishughulisha na hii biashara

2. Nunua jengo/ardhi, pangisha/kodisha/ Jenga kisha pangisha au kodisha

3. Nunua jengo/ardhi kisha endeleza/boresha kisha uza (kama jengo rekebisha choo/bafu, sakafu,paka rangi, weka umeme,weka bustani n.k kisha uza. Kama eneo, panda miti,weka uzio, weka njia ya kufika kwenye eneo n.k kisha uza)

4. Nunua ardhi/jengo kisha subiri kwa muda (mali ipande thamani/i-appreciate) kisha uza

Mambo Muhimu ya Kuzingatia katika Biashara ya 'Real Estate'

1. Katika biashara hii, unatengeneza faida wakati unanunua eneo/jengo na si wakati unauza. Kipindi cha kuuza unagundua tu faida uliyotengeza, lakini unatengeneza faida wakati unanunua. Angalau offer yako ya kwanza unapotaka kununua mali, iwe 70% au chini ya thamani halisi ya hiyo mali.

2. Eneo la ardhi/jengo lilipo ni jambo la msingi katika biashara ya 'Real Estate'. Hii inategemeana na malengo yako katika kile unachonunua, je ni kwa ajili ya biashara? makazi?

3. Jitahidi kadiri uwezavyo kujua kwanini muuzaji anauza jengo/eneo lake kabla hujataja offer yako.

4. Kwenye makubaliano jengo hoja kwa kutumia mapungufu ya 'Real Estate' ili uuziwe kwa bei ya chini

5. Sishauri utumie madalali (I'm sorry madalali), kama ukiwatumia sisitiza kukutana na mwenye mali mwenyewe.

6. Unaweza kuhusisha wataalam wa majengo au/na ardhi (kama wahandisi au wataalam wa ardhi wa eneo husika).

7. Kuwa mtulivu, usiwe na pupa (be patient). Utulivu unaweza kuokoa milioni za hela ambazo ungeweza kupoteza.

8. Kipimo cha kama umefanya biashara nzuri ni kama hela uliyotumia itarudi kati ya miaka 3-4 tangu ununue (endapo umeamua kupangisha)

9. Kuwa na hela benki 'isiyo na kazi'. Kumbuka, kuwa mtulivu katika kununua na kuuza kwenye biashara lakini sijakwambia ufanye mambo polepole. Na unaweza kununua nyumba nzuri kwa bei chee, endapo una hela ambayo ipo tayari (stand by).

Kumbuka, kuchelewa saa moja kwenye hii biashara kunaweza kukukosesha kiwanja/nyumba ambayo ingekuingizia mamilioni.

Je hii ni Biashara ya Matajiri tu?

Ni ukweli usiopingika kwamba watu kwenye kipato kikubwa wana nafasi kubwa ya kufanya hii biashara. Lakini kama hawana 'determination' bado hii biashara ni ngumu kwao. Ni rahisi Mtu wa kipato cha chini mwenye hamasa kubwa/malengo kufanya hii biashara kuliko Mtu wa kipato cha juu asiyejielewa.

Changamoto kubwa itakayompata Mtu wa kipato cha chini ni muda, kwani atahitaji muda zaidi kupata mtaji na kufanya hii biashara, KAMA ILIVYO KWENYE BIASHARA NYINGINE. Baada ya kupata jengo/eneo la kwanza, biashara itakuwa kama Mtu aliyekuwa anashikiwa baskeli ili aendeshe, sasa anaendesha mwenyewe bila kushikiwa. HAWEZI KUSHINDWA TENA KUENDESHA PEKE YAKE.

Faida ya Biashara ya Real Estate

1. Biashara rahisi ku-manage pengine kuliko zote. Utaingiza hela ukiwa mbali, ukiwa unaumwa, ukiamua kuacha kufanya Kazi (sijasema ajira, nimesema ukiamua kuacha kufanya Kazi)

2. Unaweza kutumia hizo mali kama dhamana, mfano kukopea n.k

3. Urithi mzuri kwa watoto/wategemezi

Baada ya kusema hayo, nikiri kwamba mimi sijui kila kitu, hivyo maoni yanakaribishwa ili na mimi nijifunze kupitia Uzi huu.

Asante.



Changamoto

1. Mtaji. Changamoto sio mtaji upo au haupo,changamoto ni je upo tayari kutumia mbinu za kupata wa hii biashara. Ni kweli, mtaji wa 'Real Estate' si sawa na mtaji wa genge, kwa watu wa kipato cha chini wanaweza kuhitaji miaka 5-10 ili kuweza kupata mtaji wa hii biashara.

Mtaji mwingine, ni network, ongea na watu uvae viatu. Huwezi kupata michongo kama hukai na Watendaji wa Kata Vizuri, Maafisa Ardhi, au kama hukai vijiweni.











Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kwa Tanzania ya sasa hii biashara hailipi, ndio maana watu hawawekezi pesa zao huko tena labda upepo ubadili mwelekeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unaweza kuwa na hoja, lakini labda ningeuliza tu

Je, kwa sasa ni biashara gani inayolipa? Unaweza ukose, karibu kila biashara watu watakwambia hazilipi. Ukihoji sana watu watakwambia Fanya biashara ya chakula (ni nzuri, lkn ni biashara short term)

Je, unasubiri hii biashara iwe dili ndio ununue viwanja, ujenge? Mwisho wa siku lazima maisha yaendelee na tunapaswa kuangalia mbali (kuwa na long term perspective). Kama sasa hivi sio dili, baadae itaendelea kuwa sio dili?Je unafahamu wenye viwanja/ardhi kariakoo walizipata wakati sio dili kwa wakati huo?

Tatu, je unaposema hizo biashara ni ngumu kwa sasa unamaanisha watu hawahitaji vyumba vya biashara kwa sasa? Je kwa sasa watu wanalala nje (hawapangi?) Je kwa sasa watu hawanunui viwanja/maeneo?

Mwisho wa siku, biashara huwa ina high point na low point. Hiyo isikuzuie kufanya biashara mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimependa sana huu uzi wako.
Naomba kujua kampuni zinazofanya hii kitu ambazo zinauza hisa zake
 
Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yap Ni biashara mzuri sana tena sana.
Mali za minada zinaeza kukuletea jam maana nyingi ni kama za dhulma
 
Mkuu BUSARA ZANGU Je, ni faida asilimia ngapi ungependekeza mtu aongeze kwa kila bidhaa anayozalisha akitoa gharama zote za uzalishaji, kodi, wage na usambazaji ??
 
Nimeona unaongea real estates za majengo na ardhi zaidi, labda niongeze hata mtu yeyote wa chini au wa Kati anaweza wekeza sehemu ndogo ya real estate akawa tajiri akaown, mfano kuuza buildings materials na kusupply, pia kilimo Ni bigger real estate business japo hujagusia....
 
Get the real estate concept and apply it on a smaller scenario / biz.

Mimi nimewahi fanya hii business ila kwa mfumo wa maduka / frame / vigoli kariakoo...nashika frame flan potential (nikisikia mtu anataka kuuza / kupangisha) alaf nakuja iuza (naiachia for a profit)

Huyo mteja anayekuja kuichukua nambamiza hela ya udalali na gharama za kunihamisha kwenye eneo hilo la biashara since yeye ndio mwenye shida.

Sijaifanya ile seriously (made a few number of deals) ila nimeona ina potential sana kikubwa ni kuwa na subra na pia fanya ufahamiane na wamiliki wa majengo kariakoo.

Inshort ili upige hela lazima anayekuuzia umlalie kwenye bei upate a cheaper deal.
 
Ni Biashara Nzuri ila naona ukiwa na mtaji mkubwa ni Bora zaid
 
Hii biashara lazma utumie akili sana na ufanye katka badhi ya mikoa
Mfano Arusha, Dar au Dodoma kwa mikoa mingne sikushauri kabsa
Mkoa kama mwanza unajenga nyumba nzuri kupangisha watu wanataka bei ndogo ukipiga kwa miaka mitano hela yako inakuwa hajarud hata nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…