LOVINTAH GYM
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 459
- 653
BUSINESS CYCLE OR TRADE CYCLE
Kwa kiswahili tunaweza sema ni duara la biashara.
Hili ni duara linaloonyesha maendeleo ya uchumi katika nchi au dunia kwa ujumla ambapo kuna kipindi uchumi wa nchi unakuwa mzuri na kuna mda uchumi wa nchi unayumba.
Hatua za duara la biashara
1. Depression
Hiki ni kipindi ambapo nchi au dunia inakuwa haina nuru kwenye uchumi wake, mambo yanakuwa magumu mno.
2. Recovery/Growth
Hii hatua basi nchi au dunia inakuwa imeanza kujikongoja na watu wanaanza kupata imani kuwa mambo yatakuwa mazuri mbeleni.
3. Boom/ Prosperity/Peak
Hii hatua basi uchumi unakuwa mzuri, kila mtu anakuwa na furaha sana katika hii hatua.
4. Recession
Hii hatua ni ile ambayo vitu huanza kuyumba, biashara zinaanza kutokueleweka.
CHANZO CHA BUSINESS CYCLE
Sababu za mtu mmoja mmoja (Induvidual causes)
1. Change in Demand (Mabadiliko ya uhitaji wa bidhaa)
Watu wengi wakiwa na uwezo na uhitaji wa kununua bidhaa basi biashara itakuwa nzuri (Boom)
Uwezo wa kununua bidhaa ukianza kushuka (recession)
Watu wakishindwa kabisa kununua bidhaa (depression)
Watu wachache wakianza tena kununua bidhaa (recovery)
2. Fluctuation of investment (Mabadiliko ya uwekezaji)
Mtu akianzisha biashara na ikaanza kufanya vizuri basi watu wengi watavutiwa kuwekeza.
Biashara ikianza kuleta faida kidogo wawekezaji wataanza kuongezeka (recovery).
Ongezeko la wawekezaji litafanya faida iwe kubwa (boom).
Dis economies of scale zikianza basi recession hutokea.
Watu wakiona faida za uwekezaji wao zinashuka hukimbilia kutoa pesa zao na depression hutokea.
3. Sheria za Serikali
Serikali ikipunguza kodi basi watu watakuwa na uwezo mkubwa wa kununua bidhaa, na biashara zitakuwa kwenye boom.
Serikali ikiweka kodi kubwa na vikwazo vyengine basi biashara zitayumba na kuwa kwenye depression.
Sababu za watu wengi za uwepo wa business cycle
(external causes)
1. Vita
Nchi zikiwanna vita basi ni rahisi uchumi kuyumba kwasababu hamna mtu ambaye ataendelea na biashara akihofia maisha yake.
2. Mabadiliko ya teknolojia.
Uvumbuzi wa vitu husaidia kurahisisha uzalishaji na kupunguza gharama za uzalishaj hivyo biashara hufikia boom kwasababu ya kuwa na economies of scale.
3. Majanga
Kama kukiwa na mafuriko mazao yataoza, nyumba zitabebwa na maji kwahiyo hii huyumbisha uchumi na depression hutokea, pia nchi ikiwa na neema ya mvua kiasi basi mazao huongezeka na mauzo hufanyika na nchi hufikia boom.
Huu mzunguko huathiri kuanzia mtu binafsi, taifa mpaka dunia kwa ujumla kwasababu tunategemeana.
Kwahiyo hata kama unapitia wakati mgumu jua upo katika depression ila soon utaenda kwenye recovery na mwishowe utapada kwenye boom, ukiwa kwenye boom ni rahisi kupitia recession na ukarudi kuwa depressed tena na hivyo hivyo ndio jinsi tunavyokua.
Mfano:
Ukiwa hujapata kazi au shughuli yoyote ya kufanya unakuwa kwenye DEPRESSION.
Kitendo cha kupata kazi au kuamua kuanzisha biashara basi ni RECOVERY, Basi hapa watu watakupongeza kwa kupata sehemu yaku volunteer, au internship au kuwa na office nzuri ya biashara au hata kuanza tu kuitwa kwenye interview.
Ukianza kuona faida ya shughuli unayoifanya unakuwa kwenye BOOM, mambo yakianza kuwa magumu hupati faida au huongezwi mshahara basi unakuwa kwenye RECESSION.
Ukiamua kuacha hio kazi au biashara unakuwa umerudi kwenye DEPRESSION.
Na mzunguko utaendelea hivyo hivyo.
Karibuni sana watoa hoja.
#tradecycle #businesscycle #economics #uchumi.