benn daniel
Member
- May 29, 2020
- 5
- 20
Kumekuwa na mijadala iliyoibuka hivi karibuni juu ya uwepo wa baadhi ya watu kupewa pasipoti ya kidiplomasia hapa nchini. Swali kubwa likiwa, je, watu hao wanazosifa za kupewa pasipoti hizo? Swala sio ni akina nani na Wala sina nia ya kuwajua, lengo la Uzi huu ni kutaka tuweze kujua ni akina nani wanazo sifa za kupata pasipoti hizo za kidiplomasia hapa Tanzania kulingana na Sheria ya pasipoti na hati za kusafiria ya 2002 iliyotiwa Saini na raisi wa awamu ya 3 hayati Benjamin Mkapa tarehe 31/11/2002 na kuwa Sheria rasmi.
Pasipoti ni hati au document inayotelewa na mamlaka husika ya nchi Fulani inayomuwezesha mtu kusafiri Kutoka nchi Moja kwenda nyingine. Sheria inatambua pasipoti kama Mali ya serikali.
Kulingana na Sheria tuliyokwisha kuizungumza hapo juu, Tanzania inatambua uwepo wa pasipoti za aina 7 zinazotolewa na Jeshi la uhamiaji (zamani idara ya uhamiaji). Pasipoti hizo ni:-
1. Pasipoti ya kawaida( ordinary passport). Hii anapewa raia yeyote yule atakaye kidhi vigezo kwa ajili ya kusafiria. Hii ni yetu Mimi na wewe. Rangi yake huwa ni ya bluu.
2. Pasipoti ya Utumishi (service passport). Hii wanapewa watumishi wa umma, sio walimu lakini au waajirwa wa serikali. Sheria imewataja wanaopaswa kupewa pasipoti hii kuwa ni; RC, DC, RAS, DDP, CDP, maofisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali au Brigedia Jenerali, washauri au wasaidizi binafsi wa Raisi, VP, PM na Raisi wa SMZ, kamishina msaidizi wa magereza na polisi n.k
3. Pasipoti ya Afrika Mashariki.
Hii anapewa raia yeyote yule mwenye lengo au Nia ya kusafiri ndani ya nchi jumuiya ya Afrika Mashariki. Ukitaka kusafiri Kenya, Uganda n.k tu bila kudhuru nchi nje ya jumuiya unaweza kupewa pasipoti hii. Hii pasipoti haiwezi kukufanya ukasafiri kwenda kwa Madiba.
4. Hati ya dharura ya kusafiria (emergency travel document).
Hii nayo anapewa raia yeyote yule ambaye amepata safari ya dharura nje ya nchi na kwa wakati huo hana uwezo wa kupata pasipoti, na dharura hiyo inapaswa kushughulikiwa ndani ya muda ambao haiwezekani kupata pasipoti Kutoka mamlaka husika.
5. Cheti cha utambulisho (certificate of identity). Hii anapewa mtu ambaye sio raia wa Tanzania na hana uwezo wa kupata pasipoti Kutoka nchi yake.
6. Geneva convention travel document. Hii hupewa mkimbizi aliyepata hifadhi Tanzania na ana Nia ya kusafiri nje ya Tanzania.
7. Diplomatic passport (pasipoti ya kidiplomasia). Hii anapewa mtu ambaye anahadhi ya kidiplomasia.
Kabla ya kuwajua Hawa wenye hadhi ya kidiplomasia hebu tujue faida ya pasipoti ya kidiplomasia:-
a. Hukupatia Kinga ya kidiplomasia (diplomatic immunity). Huwezi kufanyiwa lawsuit kwa baadhi ya makosa.
b. Hukupatia utambulisho unaoeleweka (clear identification).
c. Visa free entry kwa baadhi ya nchi.
d. Tax free travel.
e. Hukuepusha na baadhi ya protokali za airports.
Baada ya kujua umuhimu wa pasipoti ya kidiplomasia, ni vyema tutambue kuwa kwa Tanzania pasipoti hii huwa na rangi Nyekundu. Na humaanishi kuwa mwenye hiyo pasipoti anadafiri kwa ajili ya shughuli za serikali.
Sheria yetu imewapa watu wafuatao hadhi ya kupewa hii aina ya pasipoti:-
Raisi na maraisi wastaafu, VP, PM, Raisi SMZ, AG, CJ, Justice of Appeal, mabalozi, PS, mawaziri na manaibu wake, maofisa wa TPDF walio na vyeo vya meja Jenerali na kuendelea, IGP, CDF, magavana, Aide-de campe wa Raisi, VP na PM, msajili wa vyama vya siasa, DGTISS, DG-PCCB, speaker, karani wa Bunge, na wastaafu maraisi, VP, PM n.k
Bei ya kuapply kwa ajili ya pasipoti zetu za kawaida ni 150k, kijana kuwa na pasipoti ni muhimu.