plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,394
- 1,434
Hi Guys!
Kuna mimea ya aina nyingi na kila mmea unatabia zake tofauti tofauti kama vile tulivyo sisi binadamu au viumbe wengine. Mimea na yenyewe ina hisia na inasikia joto au baridi kama viumbe wengine walivyo.
Mimea mingi chakula chake ni maji na madini yaliyoko ardhini. Kuna mimea yenye uwezo wa kustahimili ukame ilhali mingine haiwezi. Mimea yenye uwezo wa kustahimili ukame inakuwa na mizizi mirefu ili iweze kuyafikia maji na madini ndani ardhini na mizizi yake huingia ndani zaidi na sana.
Kuna baadhi ya mimea inashangaza kidogo kwa utofauti wake ukilinganisha na mimea mingi duniani. Kuna baadhi ya mimea yenyewe inakula wadudu na viumbe wengine licha ya kuwa bado inaendelea kupata maji na madini ardhini.
Mimea inayokula wadudu na viumbe wengine kitaalamu inaitwa Carnivorous plant. Ipo ya aina tofauti tofauti lakini kwa leo tuangalie mimea inayoitwa Venus Flytrap.
Venus Flytrap kwa juu ni kama mdomo wenye meno, yenyewe inakuwa open na inavutia sana kwa wadudu na viumbe wengine kupita juu yake. Na wadudu hao au viumbe wengine wanapopita juu inajifunga inafanya digestion ikimaliza inajifungua tena kutega chakula kingine.
Mimea hii hisia yake ni kama hisia ya ngozi ya mwanadamu anavyotembelewa na mdudu. Hisia yake ni sensitive sana, hivyo inapohisi kuna kiumbe juu yake inajifunga.
Kiumbe chochote kikiwa trapped hakiwezi kuescape. Pia mimea hii inabagua chakula ikiona mdudu au kiumbe hana virutubisho vya kutosha inamruhusu kuescape.
Mimea hii inauwezo wa kula hata chura, panya, na viumbe wengine ilimradi tu apite juu yake then anabanwa na anakuwa trapped.
View attachment:
Sent using Jamii Forums mobile app