Ifahamu sheria ya Misiba ya Viongozi wa Kitaifa ya mwaka 2006

Ifahamu sheria ya Misiba ya Viongozi wa Kitaifa ya mwaka 2006

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
SHERIA YA MISIBA YA VIONGOZI WA KITAIFA YA MWAKA 2006.

Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241.

1. NANI VIONGOZI WA KITAIFA.

Kifungu cha 3, viongozi wa kitaifa ni Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Makamu wake, na Waziri Mkuu.

2. KIONGOZI WA KITAIFA ANATAKIWA AZIKWE WAPI.

Kifungu cha 16 na 17 anatakiwa azikwe Dodoma kwenye Makaburi rasmi ya Viongoz wa Kitaifa, isipokuwa akiacha wosia kuwa asizikwe hapo basi hatazikwa hapo.

3. MUDA WA KUOMBOLEZA NI SIKU NGAPI.

Kifungu cha 8( 1) , Muda wa Maombolezi na Bendera nusu Mlingoti ni Siku 21.

4.KOSA LA KUTOA SIRI ZA MAREHEM KIONGOZI WA KITAIFA.

Kifungu cha 26, Adhabu ni kifungo miezi 6 au faini Tshs 500,000 kwa kutoa siri za marehemu kiongoz wa kitaifa.

5. UTARATIBU MAZIKO NA MSIBA NI UPI .

Kifungu cha 14, atazikwa kwa taratibu za dini yake, mila na desturi.

6. KAMATI YA MSIBA NI NANI NA NANI.

Kifungu cha 11, kamati inajumuisha Waziri mkuu kama mwenyekiti wa kamati, katibu mkuu kiongozi, Waziri wa ulinzi, Waziri wa Ulinzi, Waziri mambo ya ndani, Waziri fedha,Afya,Muungano, Mwanasheria Mkuu na Cdf.

7. WAPI HESHIMA/SALAMU ZA MWISHO ZITOLEWE.

Kifungu cha 18(1), zitolewe uwanja wa Taifa Dat Es Salaam, au prnginepo.

8. MUDA WA KUTOA HESHIMA NI SIKU NGAPI.

Kifungu cha 28(2), Kamati ya msiba ina mamlaka ya kupanga muda uwe siku ngapi baada ya kushauriana na familia na viongozi wa dini.

9. NI MIZINGA MINGAPI IPIGWE.

Kifungu cha 20(3), siku ya maziko itapigwa mizinga 21 eneo karibu na sehemu alipozikwa.

10.NI LAZIMA KIGARI KINACHOBEBA MWILI KUFUNIKWA NA BENDERA.

Kfungu cha 21(1), Ni lazima kigari(bier) kinachobeba mwili ya Kiongozi kufunikwa na bendera ya taifa.

11. BENDERA INAYOFUNIKA KIGARI KINACHOBEBA MWILI KUKABIDHIWA KWA FAMILIA.

Kifungu cha 21(2), bendera inayofunika kigari(Bier) kinachobeba mwili itakabidhiwa na kutunzwa na familia ya marehemu.

12. FEDHA ZA MSIBA ZINATOKA WAPI.

Kifungu cha 23, fedha na matumizi yote yatatoka mfuko wa fedha wa Taifa(Consolidated Fund).

13. GWARIDE LINAFANYIKA LINI NA WAPI.

Kifungu cha 20, gwaride maalum litafanyika siku ya mazishi na sehemu ya mazishi na litafanywa na JWTZ.
 
Kama Kutoa Siri za Marehemu hata Wosia ni Siri pia ya Marehemu
 
Sawa Sawa
Usitokee Uchotaji Wa Fedha Kwenye
Mazishi Ya Mpendwa Wetu Magufuli
 
Hilo Bendera Watunze Familia inamaana Waliweke kwenye Masanduku au Waning'inize kwenye Mlingoti juu na kila asubuhi kuipandisha juu na Jioni Kushusha chini?

Kuna Mambo yanatakiwa kubadilishwa kwenye misheria yetu.
 
Back
Top Bottom