Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Kwa mujibu wa Shirika la Afya pamoja na Shirika la chakula na Kilimo Duniani (2018) wanaitafsiri sumu kuvu kuwa ni aina ya ukungu unaojitokeza kwenye nafaka kutokana na kuvu (fungi) jamii ya Aspergillus, Fusarium na Penicillium.
Sumu kuvu "mycotoxins" huweza kuzaliwa kwenye nafaka, matunda yaliyokaushwa na vingo(spices). Sumu hii huweza kupenda hata katika sehemu za ndani kabisa za nafaka iliyoathiriwa na kuvu.
Madhara ya sumu kuvu "mycotoxins" ni pamoja na :kuua(sumu), kudhohofisha kinga ya mwili, na saratani. Sumu hii ina madhara pia kwa wanyama.
Zipo namna nyingi za kuepukana na sumu kuvu miongoni mwa njia ni pamoja na uchambuaji mzuri wa nafaka kwa kuhakikisha nafaka zilizoathiriwa na kuvu hazichanganyiki na nafaka nzima na jambo la muhimu zaidi ni uhifadhi mzuri wa nafaka.
Tanbihi: Hii kwa wakulima wenzangu huwa tunaiona sana unaweza ukawa shahidi wa hili.