Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
- Thread starter
-
- #21
Karanga zinapendwa sana na kuvu...Asilimia kubwa ya wabongo wanaweza wasiwe exposed kwenye kiwango kikubwa cha aflatoxin na aina nyingine za sumu kuvu kutokana na kula ugali wa sembe, kukoboa mahindi kunapunguza sumu kuvu kwa kiwango kikubwa sana. Kwa wale wanaopenda dona, ni bora ukaandaa mahindi yako mwenyewe, ukaaondoa yale mahindi mabovu, ukaosha na kuanika kabla ya kwenda kusaga.
Kwa sababu karanga zinaweza kuwa na kiwango kikubwa cha aflatoxin, inafaa kuzichambua na kuondoa zile mbovu na zilizosinyaa. Kwa wale wanaoandaa unga kwa ajili ya watoto wawe makini zaidi kuchambua mahindi na karanga kwa ajili ya kusaga unga kwa ajili ya uji wa mtoto, nafikiri tumeelewana ndugu zanguni....
Ikifuatiwa na MAHINDIKaranga zinapendwa sana na kuvu...
Yaa, pamoja na mahindi, mfano, kule kenya milipuko ya watu kuugua na baadhi kufa kutokana na kula mahindi yenye kiwango kikubwa cha aflatoxin vimekua vikitokea mara kwa mara tokea mwaka 1981 na hivi karibuni mwaka 2004. Nilishangaa kusikia wanasema mahindi kutoka Tanzania yana aflatoxin jambo ambalo si kweli. Kutokana na kuwa na uhaba mkubwa wa mahindi huko kenya, watu wanaweza kuhifadhi hayo mahindi kwa muda mrefu kwenye mifuko ya sandarusi ambayo inaweza kupelekea kutengeneza uvundo na kuzalisha kiwango kikubwa cha aflatoxin, na kutokana na hali ya uhaba wa nafaka watu hasa wa kipato cha chini hawana namna ya kuacha kutumia mahindi hata kama kwa macho yataonekana hayafai kutumiwa kama chakula....Karanga zinapendwa sana na kuvu...
Karanga zinapendwa sana na kuvu...
Inawezekana lakini wameshayashuku mahindi yetu hivyo ni vyema tuwe na hii elimu ya uhifadhi bora ili kugeuka hasara.Yaa, pamoja na mahindi, mfano, kule kenya milipuko ya watu kuugua na baadhi kufa kutokana na kula mahindi yenye kiwango kikubwa cha aflatoxin vimekua vikitokea mara kwa mara tokea mwaka 1981 na hivi karibuni mwaka 2004. Nilishangaa kusikia wanasema mahindi kutoka Tanzania yana aflatoxin jambo ambalo si kweli. Kutokana na kuwa na uhaba mkubwa wa mahindi huko kenya, watu wanaweza kuhifadhi hayo mahindi kwa muda mrefu kwenye mifuko ya sandarusi ambayo inaweza kupelekea kutengeneza uvundo na kuzalisha kiwango kikubwa cha aflatoxin, na kutokana na hali ya uhaba wa nafaka watu hasa wa kipato cha chini hawana namna ya kuacha kutumia mahindi hata kama kwa macho yataonekana hayafai kutumiwa kama chakula....