Dr Rutagwerera Sr
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 5,809
- 11,462
Habari wadau wa Sports forum na JF members kwa ujumla. Sikuwa nikiwafahamu kwa undani hawa jamaa ni mpaka niliposikia taarifa kutoka kwa baadhi ya wadau na kuamaua kuwajua kwa undani ni akina nani na vipi wanahusika moja kwa moja ktk kuathiri soka la bongo.
Afrisoccer ni taasisi mpya iliyojitolea kwa dhati ktk kuhakikisha sekta ya michezo inakua kwa kasi nchini na kuifanya ya kibiashara tofauti na ilivyo sasa. Kwa kuanzia wamejikita ktk soka na baadaye ktk michezo mingine hasa riadha na ndondi. Taasisi hii inaundwa na wadau kama Bw Geoffrey Mwambe ambaye ni mchumi kitaaluma BoT, bwana Charles Palapala, Godfrey Nangu, Florian Kaijage na wengineo ambao wako nje ya nchi.
Moja ya shughuli ambayo wamedhamiria kuifanya ni kuhakikisha mikataba ya vijana wanaocheza ktk ligi za nyumbani inafanikishwa kwa kufuata taratibu na haki kwa pande zote zinazohusika. Kwa muda mrefu sasa imekuwa ni kawaida kwa vijana wetu kunyonywa na vilabu, ama kutojua kanuni na sheria zinazowaongoza ktk suala zima la mikataba na kubwa zaidi kukosa mawakala ama management za kuwasimamia.
Jambo lingine ni kuhakikisha soka letu linaendeshwa kisasa, kwa kujaribu kubuni miradi imbayo itashirikiana na vilabu vyetu kwa kuanzia vilabu vya Simba, Yanga na Azam pamoja na TFF kama shirikisho la soka. Bila kusahau na timu ya taifa.
Hadi sasa wameanza kushirikiana na vilabu hivi na ktk moja ya hatua kubwa ni mradi mkubwa ambao wanategemea kuufanya hivi karibuni ya klabu ya Yanga ambao utaipelekea Yanga kuvuna mabilioni ya fedha bila kutegemea ufadhili kutoka kwa wadhamini wao. Jambo lingine ni kuhakikisha vijana wengi wanafanikiwa kupata majaribio ya soka nje ya nchi na kwa kuanzia wapo ktk mchakato wa kupeleka vijana Spain amabapo wanahitajika kama amateur players.
Hivyo ni jambo la msingi kama wadau wa michezo na JF kuwaunga mkono ktk harakati zao na kubwa na la msingi ni ku-like facebook page yao http://www.facebook.com/afrisoccer.tanzania ili kuweza kutoa maoni na ushauri zaidi. Pia unaweza kuwapa taarifa juu ya kipaji chochote unachokifahamu chenye umri wa miaka chini ya 17, ambacho kinaweza kutengenezwa na ku-shine nje ya nchi.
Tuwaunge mkono. NAWASILISHA