Ifahamu Tanganyika kabla 1964

Ifahamu Tanganyika kabla 1964

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Tanganyika ni jina la kihistoria
Kwa sababu za kisiasa, mara nyingi huitwa "Tanzania bara" ingawa ina visiwa pia, hasa Mafia na Kilwa.

Tanganyika ilikuwa eneo lindwa la Uingereza kuanzia 1919 na nchi huru kati ya 1961 hadi 1964, mwaka wa kwanza kama ufalme, halafu kama jamhuri.

Mwaka 1964 iliungana na Zanzibar na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Chanzo katika koloni la Kijerumani

Maeneo yaliyoitwa baadaye (1920) "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni la Ujerumani lililoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila.

Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.

Tangu mwaka 1885 Karl Peters, kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wenyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha na Ukami iliyoweka msingi wa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo hayo.

Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.

Koloni lile la Kijerumani lilikuwa kubwa kuliko Tanganyika ya baadaye, maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hilo la Kijerumani lilitekwa na majeshi ya Uingereza na Ubelgiji.

Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua makoloni yote ya Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mikononi mwa Ubelgiji.

Tanganyika Territory ya Kiingereza baada ya kuondoka kwa Wajerumani

Mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles.

Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithibitisha hatua hiyo na kuamua masharti ya kukabidhi.

Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni hilo na tangu Januari 1920 wakaamua kuliita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

Katika Vita vikuu vya pili, wananchi 100,000 hivi waliungana na jeshi la Uingereza[2] wakiwa kati ya Waafrika 375,000.[3] Watanganyika walipiga vita katika vikosi vya King's African Rifles huko Somalia, Uhabeshi, Madagascar na Burma.[3] Pia Tanganyika ilikuwa chanzo kikubwa cha chakula[2] Jambo hilo lilisababisha mfumuko wa bei usio wa kawaida
 
Umenikumbusha mbali sana mr eden.KINGS AFRICAN RIFFLES
 
wenyewe watanganyika ukitaja jina la tanganyika unawarusha stim zote,huu uzi hawatauchangia hata kidogo hawataki kuliona hilo jina kabisa,yaani kama aibu kwao kuitwa mtanganyika,ajabu sana hata hawataki kujua historia ya tanganyika,wao wamelewa na tanzannia tu na historia wanayoitambua ni kuanzia mwaka 64 na muungano
 
Hapo unakosea mie mtanganyika nachukia muungano usiokuwa na faida zaidi kelele kila siku japo ndugu zangu upande wa pili hataki muungano pia ila kutwa kuwekeza tanganyika hapo ndipo nisipo waelewa...
 
wenyewe watanganyika ukitaja jina la tanganyika unawarusha stim zote,huu uzi hawatauchangia hata kidogo hawataki kuliona hilo jina kabisa,yaani kama aibu kwao kuitwa mtanganyika,ajabu sana hata hawataki kujua historia ya tanganyika,wao wamelewa na tanzannia tu na historia wanayoitambua ni kuanzia mwaka 64 na muungano
Tanzania si baada ya kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar
 
Back
Top Bottom