Ifamu ugonjwa wa Kiharusi (Stroke), Dalili na Matibabu:

Ifamu ugonjwa wa Kiharusi (Stroke), Dalili na Matibabu:

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
327
Reaction score
537
Kiharusi (stroke) ni ugonjwa wa kupooza sehemu au upande mmoja wa mwili kutokana na hitilafu/uharibifu kwenye ubongo, hasa ubongo kukosa damu au damu kuvilia ndani ya ubongo.
Kiharusi husababisha ulemavu na vifo duniani kote ambapo kila mtu mmoja (mwenye miaka 25 na zaidi) kati ya wanne hupata kiharusi katika maisha yao.

Stroke (Kiharusi) husababishwa na damu kuvuja kwenye ubongo (hemorrhagic stroke) au sehemu ya ubongo kukosa damu na hivyo kufa (ischemic stroke).

Kiharusi cha damu kuvuja (hemorrhagic stroke) mara nyingi dalili zake huanza ghafla baada ya mishipa ya damu kupasuka ambapo mtu hupooza upande mmoja wa miwili.

220px-Parachemableedwithedema.png

Damu iliyovilia kwenye ubongo (hemorrhagic stroke: utando mweupe, angalia mishale)

Kiharusi cha ubongo kukosa damu (ischemic stroke) kutokana na mishipa ya damu kuziba na dalili zake huanza taratibu kwa mtu kupata udhaifu katika mkono na mguu wa upande mmoja na hatimaye hupooza kabisa kama hatua hazitachukuliwa mapema.

220px-MCA_Territory_Infarct.svg.png

Sehemu ya ubongo iliyokufa (ischemic stroke: utando mweusi, angalia mshale)

Pia wengine wanaweza kupata aina zote mbili (hemorrhagic na ischemic strokes) hasa pale ambapo mishipa imeziba (ischemic stroke) na wakati mwingine kupasuka (hemorrhagic stroke).

Visababishi:
-matatizo ya damu kuganda (clotting disorders) husababisha mgando ambao huziba mishipa ya damu
-viwango vikubwa vya mafuta kwenye damu (atherosclerosis)
-magonjwa ya moyo mfano mshituko, nk
-shinikizo la juu la damu (high blood pressure)
-magonjwa mengine ya ubongo mfano uvimbe kwenye ubongo nk

Dalili za Kiharusi (stroke):
-ugumu au kushindwa kutembea au kutumia mkono
-kupooza upande mmoja wa mwili
-ugumu kwenye kuongea au kushindwa kabisa kuongea
-mdomo kwenda upande mmoja
-kuwa na uoni hafifu au uoni kupotea kabisa, kuona giza au kizunguzungu nk
-kupata ganzi na udhaifu kwenye miguu
-kushindwa kumeza chakula, kuchanganyikiwa nk

Vipimo:
Ili kubaini aina ya kiharusi ni lazima mgonjwa afanyiwe kipimo cha kuangalia ubongo, CT scan Brain 🧠 ambacho huonesha sehemu ya ubongo iliathiriwa. Majibu ya kipimo hiki ndiyo husaidia katika kuamua aina ya matibabu ambayo mgonjwa atafaidika nayo.
Pia vipimo vingine vya damu vinaweza kufanyika.

Matibabu:
Matibabu ya kiharusi (stroke) huwa katika kutoa dawa za kushusha shinikizo la juu la damu ( high blood pressure) hasa kama damu ime/inavuja kwenye ubongo (hemorrhagic stroke) na dawa za kufanya damu ifikie ubongo kwa urahisi (blood thinners) hasa kama mishipa ya damu zimeziba (ischemic stroke) nk.

Matibabu ya upasuaji hasa kwa kiharusi cha damu kuvuja kwenye ubongo (hemorrhagic stroke) ambapo damu iliyovilia kwenye ubongo hutolewa, lakini upasuaji huu hutegemea kiwango cha damu, sehemu ilipovilia, muda uliopita tangu damu ianze kuvuja, athari iliyotokea kwa mgonjwa na hali ya afya ya mgonjwa (stability).

Pia kwa kiharusi cha mishipa kuziba (ischemic stroke) kuna upasuaji wa kuzibua mishipa hiyo kuondoa mgando ulioziba (mechanical thrombectomy) ili kuruhusu damu kupita kwa urahisi. Upasuaji huu unafanyika katika hospitali/nchi ambazo wana vifaa maalumu ya kufanyia upasuaji huo.

Mbali na dawa na pengine upasuaji mgonjwa pia hufanyiwa mazoezi maalumu ya viungo (physiotherapy) kama sehemu ya tiba ili kufanya sehemu za mwili zilizoathiriwa ziweze kurudi katika hali ya kawaida ya utendaji kazi. Mgonjwa anakuwa na kiliniki ya mazoezi hayo kila siku/wiki au mwezi kulingana na hali yake na uhitaji.

Ni muhimu kuchukua hatua mapema kwa:
-kuhakikisha unapima shinikizo lako la damu (blood pressure) walau mara kwa mara
-kuhakikisha unazingatia dawa za pressure kama umegundulika na tatizo la shinikizo kubwa la damu (hypertension).
-kuzingatia mazoezi na mlo kamili
-kuepuka matumizi ya pombe na sigara.
 
Naogopa kupata kiharusi, sitaweza kufanya mapenzi na mke wangu
 
Back
Top Bottom