Agosti 5, 2026, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeomba radhi kutokana na makosa yaliyofanywa katika mchakato wa pendekezo lililoondolewa la kuuza haki za kibiashara zinazohusiana na Kombe la Dunia. Wakati huohuo, viongozi wa shirikisho hilo wamethibitisha tena kumuunga mkono rais wake, Gianni Infantino, kufuatia kikao cha dharura kilichofanyika mjini Rabat, Morocco.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Infantino, Katibu Mkuu wa FIFA Mattias Grafström pamoja na wajumbe wa bodi ya usimamizi wa FIFA. Baada ya mkutano huo, FIFA ilisema viongozi wake wamethibitisha kumuunga mkono kikamilifu rais huyo, huku wakikiri kuwa namna pendekezo la FIFA Forward Enterprise lilivyoshughulikiwa ilipaswa kuwa tofauti.
Soma Rais wa FIFA Gianni Infantino aitisha kikao cha dharula
Katika taarifa yake, FIFA ilisema pia imetuma barua tofauti kwa wajumbe wa Baraza la FIFA na mashirikisho yote 211 wanachama wake, ikiomba radhi kwa makosa yaliyotokea na kuahidi kufanya tathmini ya kina ya mchakato huo.
FIFA iliongeza kuwa baada ya pendekezo hilo kuondolewa, haitavumilia tena mashambulizi yoyote dhidi ya uadilifu wake, misingi ya utawala bora na taratibu zake za maamuzi, na kwamba itachukua hatua zote muhimu kulinda hadhi na sifa yake.
Kikao hicho kilifanyika baada ya FIFA kuondoa wiki iliyopita pendekezo la kuuza asilimia 20 ya hisa katika kampuni mpya ya kusimamia haki za kibiashara kwa wawekezaji binafsi. Mpango huo ungeiwezesha FIFA kukusanya takribani dola bilioni 4.2 kwa ajili ya maendeleo ya soka duniani. Pendekezo lililozua mjadala kutokana na kuhusishwa kwa kampuni yenye uhusiano wa kifamilia na Rais wa Marekani Donald Trump.
Hatua hiyo ilikosolewa vikali na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) pamoja na wadau wengine wa mchezo, ambao waliishutumu FIFA kwa kukosa uwazi, utawala bora na kushindwa kufanya mashauriano ya kutosha kabla ya kuwasilisha mpango huo.
Chanzo: Reuters