Kupigana na Nafsi!! ni LEO, Kesho ni kubahatisha.
Mema yatende LEO, Usiseme kesho itafika.!
Mola kakupa LEO, Kesho bado kaificha.
Udumu kutenda LEO, Kesho huna uhakika.
Tufanye mema kwa LEO,maisha ni kubahatisha.
Inuka uswali LEO kesho haija fika.
Wakumbushe wengine LEO pengine kesho hutofika
Udumu kutenda LEO, Kesho huna uhakika