Mhhhh! Kwanini G!?
I don't know. It just does
Haikutokei wewe kusikia labda ala tupu za muziki au nyimbo bila ya kujua maana na ikakufanya sad? Na mbaya yake nakuwa siwezi kuizima mpaka niisikie yote (@-@)
Mimi ni vice versa naupenda sana wimbo huu, kama wewe nikiusikia basi sitaki kuishia kati husubiri hadi uishe huwa unanikumbusha Samora Machel kiongozi ambaye nilimpenda sana baada ya Mwalimu. Kuna nyimbo hasa za ala tupu nikisikia huwa sitaki niondoke mpaka ziishe hasa za yule Andrea Bocelli.
Huu wimbo umeelekea kama upigwe kwenye mazishi hivi au watoto wanaokufa njaa. Hiyo ndo image nnayopata nikiusikia
Sina uhakika lakini inaweza kuwa mara ya kwanza kuniingia akilini ilikuwa alipokufa Samora Machel kwa hiyo nauhusisha na vifo na sadness
Huu wimbo unanikumbusha mbali sana wakati wa ukombozi kusini mwa Afriika.
Wimbo huu kwa hisani ya emwandosya wa YOUTUBE:
Inatukumbusha jinsi Tanzania ilipokuwa kimbilio la wanamapinduzi wakaweka makazi yao Tanzania mfano Samora Machel, Eduardo Mondlane n.k na wazazi wangu waliupenda sana wimbo huu naambiwa ikiwemo Mzee Moses Mnauye na watoto wa halaiki.
Ni kweli mkuu sisi tuliosoma kitambo.masopakyindi ,
..Samora Machel alikufa October 19, 1986.
..sasa hivi kuna video clips nyingi zinazomhusu Samora Machel ziko kwenye mtandao.
Samora alikuwa our super hero tukiwa mashuleni, haswa wakati wa vita ya ukombozi.
Mkuu MODS watoto wa juzi...hivi tatizo ni macho yangu, au?
..kwamba uzi huu uko kwenye jukwaa la " "entertaiment"!!
Cc masopakyindi , Nguruvi3
Mkuu MODS watoto wa juzi.
Tunachojadili inaelekea aidha hawakijui au ni historia iliyowapita.
Sisi wengine tukisikia kina Samora Machel, Josina Machel, Eduardo Mondlane, Marcelino Dos Santos, ZJoachim Chissano, Mapande na wengine wengi, damu za kimapinduzi zinachemka tukikumbuka ujana wetu wa 60/70's.