Ifike mahala mtushukuru sisi mafisadi

kingkongtz

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2019
Posts
1,058
Reaction score
3,613
Nakumbuka miaka ya nyuma Hali ilikuwa nzuri na ya kuridhisha kwel kweli,licha ya upigaji wa maeuro/mapound tulokuwa tunaminya bado Hali mtaani ilienendelea kuwa fresh ukilinganisha na sasahivi.

Zaman tulipiga sana pesa na kujenga vitu ambavyo vilikuw ajira kwa vijana mitaani,(Leo hii kijana wa miaka 27+ anashindwa kujitegemea kisa ukata wa maisha)

Pesa tulizokuw tunachapa japo sasahivi tunaonekana wabaya (wahujum uchumi),zilifanya mfumo wa maisha ukaenda smooth sana japo sio kwa wote ila 67% walinufaika.

Zaman ulikuw ukikuta kwenye miradi yetu kama hospital,vyuo,shule,kampuni tumeajir vijana,wafanyabiahsara Mambo yalikuw super,

Wanawake waliolewa na wenye pesa kwa hyo maisha yalibalance kiaina
Leo mdada 29+ unataman kuolewa ilawaoaji hawapo maisha yameban kishenzi

Vijana weekend ulikuw ukiwakuta beaches wakiinjoy baada ya kuingiza mpunga mrefu plus kuwawezesha madem zao,Leo hii mnaviziana Kama kunguni

Kesi mahakamani UKiwa na chochote ulikuw unashinda,(wale waliobambikiziwa kesi wamenielewa)

Vitu vilikuw Bei Chee kwel kwel hakuna mwananchi alokuw akilalamika Mara sukari Mara ngano Mara cement kupanda Bei ghafla,

Biashara ya mazao pia ilikuw ikienda kas sana (leo hii naskia ukikamatwa unapeleka chakula nje unauliwa Kama Gaddafi)how come mkulima apangiwe Cha kufanya??

Tumenunua magari mengi vijana tukawaachia vijana wapige Kaz wajipatie kipato.

Ulikuw ukilipa ada shulen unasema ewaa !! mim kwel mwanaume,Leo hii et elimu bure kweli?? (mwanaume na kitu Cha bure wap na wap)

Kutajirika kulikuw nje nje kwa vijana Mana madeal yalikuw mengi kishenz.unakuta miaka hiyo kijana wa miaka 27 anamjengo wa ukwei,(kijana wa Leo Yuko kwa mzaz anaangalia hotuba "NILETEENI GWAJIMA")

Nakumbuka miaka hyo vijana weng wamenunua magari,wamejenga,NK
Leo hii unafungua duka la m10+ kesho kutwa limekufa coz Amna wanaonunua pesa kitaa hamna(wapo ila kidogo)

Nimechoka kuandika araaa.ngoja nimalizie kvant next week niagize TATA nyingne

VIJANA PAMBANENI HIVYO HIVYO NA MMPE MI5 TENA.SISI TULITUMBULIWA HUKU TUMEWEKEZA NJE ,TITEGEMEA TULE NA NYIE ILA NGOJA TUENDELEE KUSWAGA RAHA .

" OUT"
 
Mafisadi mlikuwa na uwezo wa kula tunda kimasihara .....but sio kwa siku hizi😁😁
 
Nimtag Mkuu??
 
Mafisadi mlikuwa na uwezo wa kula tunda kimasihara .....but sio kwa siku hizi[emoji16][emoji16]
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Umenena vema fisadi
 
Nyie mafisadi ndiyo mmetuponza..

Nasikia Jamaa mlikuwa mnamdharau, sasa ameshika mpini anadhani anawakomesha nyie, tunaumia sisi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…