Ifike mahali kama taifa tuseme hapana kwa yale ambayo sio kipaumbele chetu

Ifike mahali kama taifa tuseme hapana kwa yale ambayo sio kipaumbele chetu

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Hebu fikiria kuna wananchi wanafurahia kupandishwa ndege na kwenda kutalii nje ya nchi. Na wengine kupewa ahadi za kuwa viongozi. Wengine kusafirishwa kwa kupanda treni mpya. Naandika haya huku nikitokwa machozi.

Watanzania wenzangu, itatusaidia nini kwenda china na kurudi na kukuta miundombinu nchini kwetu ni mibovu? Baadhi ya barabara hazipitiki kwa mwaka mzima hasa wakati wa mvua. Wanafunzi wengine wanakaa chini kwa kukosa madawati.

Wananchi wanakosa huduma za afya ikiwa hawana fedha za matibabu. Baadhi ya watumishi hawana makazi, wanaishi nyumba za kupanga zilizo mbali na maeneo yao ya kazi. Nchi haina viwanda vya kutosha. Ajira hakuna, zikitoka ni kwa uchache.

Halafu wewe mwalimu unafurahia kusafiri kwa SGR kutoka Dar kwenda Morogoro? Au wewe kijana (UVCCM) unafurahia kusafiri kwenda China, Korea n.k kutalii. Huoni uchungu kwa Wananchi wa hali za chini kukatwa kodi na tozo?

Maskini nchi yangu! Mwenyezi Mungu aliponye taifa hili.

Binafsi siko tayari kuingia kwenye huu mtego. Siko tayari kushiriki dhambi za mtu mwingine kwa kuvaa tshirt na kubeba bango la kusifia ilihali Wananchi wengi wanalia kwa mfumko wa bei.

Tozo kila mahali.Wao Viongozi na machawa, kila kukicha ni kutalii tu nakutumia tozo kiholela. Nasema siko tayari hadi pale yanaylalamikia yapatiwe ufumbuzi. Hapo ndipo nitakuwa tayari kuunga mkono juhudi zake.
 
Wewe unataka serikali ifanye nini.? Unataka serikali ikujengee barabara ya kutoka chumbani kwako kwenda chooni kwako..? Tupinge vinavyopingika sometimes..
Ndugu, si kila anayeandika thread ya kukosoa kile kinachofanywa na serikali ni mpinzani wa serikali. Kuna wengine ni wazalendo wa kweli. Hatudanganyiki kwa ahadi au trip za nje au ndani ya nchi.

Tunachohitaji ni matumizi sahihi ya kodi zetu. Matumizi yenye tija kwa taifa na sio kwa maslahi ya wachache.
 
Back
Top Bottom