Ifike mahali Serikali ilinde majina ya taifa: Si kila mtu aruhusiwe kusajili kampuni kwa majina ya Kilimanjaro, Serengeti, Simba na mengineyo

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Kuna jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likinisumbua.

Leo hii unaweza kupita barabarani ukakuta Kilimanjaro Company Ltd, Serengeti Traders, Simba Enterprises, Safari Logistics, Ngorongoro Supplies na majina mengine mengi yenye uzito mkubwa kwa taifa.

Kwangu, hili si suala la kawaida. Naona ni wakati sasa serikali itazame upya utaratibu wa kuruhusu matumizi ya majina yenye alama na utambulisho mkubwa wa Tanzania.

Majina kama Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Zanzibar, Ruaha, Selous, Simba na mengine yanawakilisha historia, urithi, utalii na taswira ya nchi yetu duniani.

Lakini ukiingia kwenye mfumo wa usajili wa biashara wa BRELA na kutafuta baadhi ya majina hayo, utakutana na kampuni nyingi sana zinazoyatumia. Kwa mtazamo wangu, hali hii imefanya majina hayo yapoteze upekee wake.

Siamini kwamba kila jina lenye thamani ya kitaifa linapaswa kuwa wazi kutumiwa na mtu yeyote bila kuwepo masharti maalum au mipaka ya matumizi.

Fikiria kwa mfano...

Kama jina Kilimanjaro lingekuwa linatumika kwa utaratibu maalum, au Serengeti lingepewa ulinzi wa kipekee, usingeona hadhi yake ikiongezeka zaidi?

Nchi nyingi hulinda kwa umakini alama, majina na utambulisho unaobeba heshima ya taifa lao. Hii husaidia kuyafanya yaendelee kuwa ya kipekee na yenye thamani kubwa.

Sidhani kama lengo ni kuwazuia watu kufanya biashara. Lengo ni kuweka utaratibu unaolinda hadhi ya majina yanayoiwakilisha Tanzania.

Labda yafanyike mambo kama:

  • Kuwe na orodha ya majina ya kitaifa yanayopaswa kulindwa.
  • Matumizi yake yaruhusiwe kwa vigezo maalum au kwa kibali maalum.
  • Yasitumike kiholela kwenye kila aina ya biashara.

Huu ni mtazamo wangu, na najua unaweza kutofautiana na wa wengine.

Je, wewe unaonaje? Serikali inapaswa kuweka mipaka katika matumizi ya majina yenye uwakilishi mkubwa wa taifa kwenye usajili wa kampuni na majina ya biashara, au utaratibu uliopo unafaa?
 
Huu ni umasikini wa fikra

Majina tu ndio yawe special hadi yasiguswe,

Majina hayo ambayo kodi tunazokatwa ndie yanaendesha shughuli zao

Majina ambayo yalikuwepo hata kabla mamlaka hazijaundwa.
 
Huu ni umasikini wa fikra

Majina tu ndio yawe special hadi yasiguswe,

Majina hayo ambayo kodi tunazokatwa ndie yanaendesha shughuli zao

Majina ambayo yalikuwepo hata kabla mamlaka hazijaundwa.
Majina kuwepo tangu enzi na enzi, sio hoja. Hapa tungaazia kulinda hadhi sio kila mtu kujiamulia tuu kutumia atakavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…