uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Habari zenu wana jamvi.
Kwa muda mrefu sasa nimeangalia wahitimu wa vyuo mbalimbali waliofanikiwa kupata ajira na ambao bado wanalazimika kulipa mikopo waliyokopeshwa na serikali ili kufikia ndoto zao za elimu. Jambo ambalo mimi binafsi naliona ni jema kwa kuwa wanafanya mfuko huo uweze kuishi ili uwasaidie na wengine.
Kitu kinachoshangaza ni pale ambapo wanatakiwa kutoa na riba kwa kiasi cha fedha ambacho bado hakijalipwa.
Pendekezo langu kwa serikali ni kwamba,kwa kuwa huyu mhitimu analipa kodi kutoka kwenye mshahara wake basi asilazimike kulipa riba alipe kiasi alichokopeshwa tu,ikiwa na maana kwamba serikali kwa kumsomesha imepanua wigo wa walipakodi na hivyo kuongeza mapato.
Jambo hilo litampatia unafuu wa maisha mhusika ukitilia maanani ndo kwanza ameanza maisha.
Kupitia hizo kodi zinazokusanywa,serikali iwe inajazia (inflation rates) kwenye mfuko wa bodi ya elimu badala ya mzigo huo kuelekezwa kwa mwajiriwa huyu mpya.
Kwa maoni yangu jambo hili litaongeza ufanisi kazini,kwa wahusika kufanya kazi bila msongo wa mawazo na pia kuepusha tamaa za rushwa zinazochochewa na kipato kutokidhi mahitaji ya mhusika.
Nawasilisha.